Wanamichezo wa Michezo ya majeshi
kwa Nchi za Afrika Mashariki wakiingia Uwanjani wakati wa Ufunguzi wa
Michuano hiyo uliofanyika katika Uwanja wa Amahoro Kigali Nchini Rwanda
Picha na (Selemani Sem unyu).
Waziri wa Ulinzi wa Rwanda
Jenerali James Kabarebe (wa pili Kulia) akifuatilia jambo wakati wa
ufunguzi wa Michuano ya majeshi kwa nchi za Afrika mashariki katika
Uwanja wa Amahoro Kigali nchini Rwanda (Picha na Selemani Semunyu)
Waziri wa Ulinzi wa Rwanda
Jenerali James Kabarebe (wa pili Kulia) akifuatilia jambo wakati wa
ufunguzi wa Michuano ya majeshi kwa nchi za Afrika mashariki katika
Uwanja wa Amahoro Kigali nchini Rwanda (Picha na Selemani Semunyu)
Baadhi ya maofisa na Wanamichezo
wa Michezo ya majeshi kwa Nchi za Afrika Mashariki wakifuatilia Ufunguzi
wa Michuano hiyo uliofanyika katika Uwanja wa Amahoro Kigali Nchini
Rwanda Picha na (Selemani Sem unyu).
Wanamichezo wa Tanzania Mashariki
wakiingia Uwanjani wakati wa Ufunguzi wa Michuano hiyo uliofanyika
katika Uwanja wa Amahoro Kigali Nchini Rwanda Picha na (Selemani Sem
unyu).
Baadhi ya Askari wa JWTZ
wakifuatilia Ufunguzi wa Michuano ya majeshi kwa Nchi za Afrika
mashariki uliofanyika katika Uwanja wa Amahoro Kigali Nchini Rwanda
Picha na (Selemani Sem unyu).
Wanarianda walioshiriki mashindano
ya majeshi kwa nchi za Afrika mashariki wakichuana wakati wa
Mashindano hayo kwa Mbio za nyika Wanawake ambapo Tanzania imeshika
nafasi ya Tatu.(picha na Selemani Semunyu)
………………………………………………………………………………….
Na Seleamani Semunyu JWTZ.
Mashindano ya majeshi
kwa Nchi za Afrika mashariki yameingia Siku yake ya kwanza baada ya
kuzinduliwa huku Tanzania ikishika nafasi ya tatu katika Riadha kwa
wanawake katika mbio zilizokuwa na Ushindani Mkali na kufanyika katika
Uwanja wa APRC Kicukiro. .
Mtanzania Catherine
Lange aliiwezesha Timu ya JWTZ kuibuka na Ushindi wa tatu huku kwa
Wanaume Mwanariadha Fabiano Nelson kufanya vyema licha kukosa ushindi
wa jumla kutokana na kuwa peke yake mbele nyuma ya wakenya waliochukua
ushindi wa Kwanza.
Awali akifungua
mashindano hayo Waziri wa Ulinzi wa Rwanda Jenerali James Kabarebe
amewapongeza Wakuu wa Majeshi Kutoka Nchi za Afrika Mashariki kwa
kuendeleza michezo na kutoa nafasi kwa nchi zo kushiriki katika
mashindano ya Afrika Mashariki ambayo yamekuwa kiungo katika kuimarisha
Ushirikiano.
Aliyasema hayo leo wakati
akizindua wa michezo hiyo katika Sherehe zilizofanyika katika Uwanja wa
Amahoro Kigali Nchini Rwanda na Kuhudhuriwa na Viongozi mbalimbali wa
Majeshi kutoka majeshi ya Nchi Nne zinazoshiriki Michuano hiyo.
“ Michezo ni Sehemu ya Majukumu
ya Jeshi Lakini nawapongeza na kuyapa uzito mashindano haya kwani
yamekuwa yakitusaidia katika kuimarisha ushirikiano wa Nchi hizo ili
kuhakikishia inaendelea kuwa sehemu salama.
Waziri Jenerali Kabarege alitoa
Wito kwa Wakuu hao kutumia nafasi ya Michezo hii kufanyia kazi
changamoto kama zipo zinazokabili majeshi katika ukanda huu.
Awali Mkuu wa majeshi wa Rwanda
Jenerali Patrick Nyamvumba aliwahahakikishia Wanamichezo maandalizi
Mazuri na kuwataka kuwa huru na kuchanganyika na Wanyarwanda ambao
alidai wameajiandaa kuwapokea.
Kwa upande wake Mwakilishi wa
Mkuu wa majeshi ya Ulinzi wa Tanzania ambaye ni Mkuu wa mafunzo na
Utendaji Kivita Meja Jenerali Issa Nassoro amesema anamatumaini makubwa
kwa Timu za Tanzania kurejea na vikombe.
Tags
MICHEZO KIMATAIFA