Waziri wa Habari ,Utamaduni,Sanaa
na Michezo Mhe.Nape Mosses Nnauye (Kushoto) akijadiliana jambo na Rais
wa China Public Diplomacy Association Bw. Li Zhaoxing(kulia) kabla ya
kuanza kwa mkutano wa China-Afrika Public Diplomacy Forum leo jijini Dar
es Salaam.
Waziri wa Habari ,Utamaduni,Sanaa
na Michezo Mhe.Nape Mosses Nnauye (katika) akipokea zawadi kutoka kwa
Rais wa China Public Diplomacy Association Bw. Li Zhaoxing(kulia) kabla
ya kuanza kwa mkutano wa China-Afrika Public Diplomacy Forum leo jijini
Dar es Salaam kushoto kwake ni Balozi wa China nchini Bw.Lv Youqing.
Waziri wa Habari ,Utamaduni,Sanaa
na Michezo Mhe.Nape Mosses Nnauye akiwasilisha hotuba yake wakati wa
ufunguzi wa mkutano wa China-Afrika Public Diplomacy Forum leo jijini
Dar es Salaam ulikuwa ukijadili masuala mbalimbali ya ushirikiano baina
ya Bara la Afrika na China.
Rais wa China Public Diplomacy
Association Bw. Li Zhaoxing akiwasilisha hotuba yake wakati wa ufunguzi
wa mkutano wa China-Afrika Public Diplomacy Forum leo jijini Dar es
Salaam ulikuwa ukijadali masuala mbalimbali ya ushirikiano baina ya Bara
la Afrika na China.
Mshauri wa mambo ya Mawasiliano
kutoka Tume ya Umoja wa Afrika Bibi. Doreen Apollos akisoma hotuba yake
wakati wa ufunguzi wa mkutano wa China-Afrika Public Diplomacy Forum leo
jijini Dar es Salaam. Mkutano huo umejikita katika kujadili uhusiano wa
Afrika na China kupitia Nyanja mbamilmbali ikiwemo mawasiliano na afya.
Waziri wa Habari ,Utamaduni,Sanaa
na Michezo Mhe.Nape Mosses Nnauye (kushoto) akijadiliana jambo na Rais
wa China Public Diplomacy Association Bw. Li Zhaoxing(kulia) wakati wa
mkutano wa China-Afrika Public Diplomacy Forum leo jijini Dar es Salaam.
Mkutano huo umejikita katika kujadili uhusiano wa Afrika na China
kupitia Nyanja mbamilmbali ikiwemo mawasiliano na afya.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe.
Paul Makonda (wa kwanza kulia) na Balozi wa China nchini Bw. Lv
Youqing(wa pili kulia) wakisikiliza hotuba iliyokuwa ikitolewa na mgeni
rasmi ambaye ni Waziri wa Habari ,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe.Nape
Mosses Nnauye(hayupo katika picha) wakati wa ufunguzi wa mkutano wa
China-Afrika Public Diplomacy Forum leo jijini Dar es Salaam.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe.
Paul Makonda (kushoto) na Balozi wa China nchini Bw. Lv Youqing(kulia)
wakionyesha hundi ya shilingi milioni arobaini na tano zilizotolewa na
watu wa China kwa ajili ya kuchangia madawati katika shule za msingi za
Dar es Salaam.
Waziri wa Habari ,Utamaduni,Sanaa
na Michezo Mhe.Nape Mosses Nnauye (katikati waliokaa ) akiwa katika
picha ya pamoja na baadhi ya wajumbe wa mkutano wa China-Afrika Public
Diplomacy Forum leo jijini Dar es Salaam.
Wajumbe wakifuatilia hotuba
mbalimbali zilizokuwa zikitolewa na wageni waalikwa wakati wa mkutano wa
China-Afrika Public Diplomacy Forum leo jijini Dar es Salaam.
Picha na Lorietha Laurence-WHUSM.
………………………………………………………………………………………………..
Na Lorietha Laurence-WHUSM
Waziri wa Habari ,Utamaduni,Sanaa
na Michezo Mhe.Nape Mosses Nnauye amewataka waandishi wa habari kuwa
wazalendo kwa kuandika habari za maendeleo ya bara la Afrika.
Hayo ameyasema leo jijini Dar es
Salaam wakati wa ufunguzi wa mkutano wa China-Afrika Public Diplomacy
Forum na kueleza kuwa uhusiano baina ya Afrika na China ni wa muda mrefu
na umejikita katika kuboresha teknolojia ya mawasiliano na hivyo kukuza
uchumi wake.
Aidha aliongeza kuwa ili bara la
Afrika liweze kuelezea historia yake kwa mataifa mingine katika
kujiletea maendeleo kuna haja ya kuvijengea uwezo vyombo vya habari
katika kutoa habari nzuri zenye manufaa kwa jamii husika.
“Katika karne hii tuliyopo sasa
kuna mabadiliko mengi ya teknolojia hivyo ni budi kuendelea
kuimarisha ushirikiano ulipo baina ya China na Afrika ili kuleta
maendeleo chanya kwa jamii zetu kupitia vyombo vya habari huku
tukitunza na kueneza tamaduni zetu” alisema Mhe.Nape.
Waziri Nape alizidi kufafanua kuwa
vyombo vya habari katika nchi za bara la Afrika vina uwezo mkubwa wa
kukuza na kueneza utamaduni, kuhudumia jamii,kujenga umoja wa kitaifa
na kulinda maslahi ya jamii duniani.
Naye Rais wa China Public
Diplomacy Association Bw. Li Zhaoxing amesema kuwa anafurahishwa na
uhusiano uonaozidi kuimarika baina ya nchi za Afrika na China na
kuahidi kuboresha mawasiliano na mahusiano ili kufikia mafanikio makubwa
yaliyokusudiwa.
Mkutano wa China-Afrika Public
Diplomacy Forum umejikita katika kujadili mambo mbalimbali ikiwemo
mahusiano baina ya mtu na mtu na Vyombo vya habari,afya,na tiba asilia.
Tags
HABARI KITAIFA