RAIS wa Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli amefanya mabadiliko
madogo ya uongozi na kumteua Bw. Mrisho Gambo kuwa Mkuu wa Mkoa wa
Arusha kuanzia leo (Alhamisi, Agosti 18,2016).
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amesema Bw. Gambo anachukua nafasi ya aliyekuwa Mkuu wa Mkoa huo, Bw. Felix Kijiko Ntibenda ambaye uteuzi wake umetenguliwa.
Amesema Bw. Ntibenda anahamishiwa Ofisi ya Waziri Mkuu ambako atapangiwa majukumu mengine.
Kabla ya uteuzi huo, Bw. Gambo alikuwa Mkuu wa Wilaya ya Arusha. Ataapishwa kesho (Ijumaa, Agosti 19, 2016) saa 3 asubuhi Ikulu jijini Dar es Salaam.
IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
2 MTAA WA MAGOGONI,
S. L. P. 3021,
11410 DAR ES SALAAM.
ALHAMISI, AGOSTI 18, 2016.
Tags
HABARI KITAIFA
