Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Mhe.John
Mongella (kulia) akitoa taarifa ya ujio wa Rais Magufuli mkoani Mwanza.
Kushoto ni Katibu Tawala mkoani Mwanza, CP.Clodwig Mtweve.
……………………………………………………………………
Judith Ferdinand, Mwanza
Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe.Dkt.John Pombe Magufuli, anatarajia kufanya ziara fupi ya kikazi mkoani Mwanza.
Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, John
Mongella, leo amesema, Rais Magufuli atafanya ziara ya siku mbili
kuanzia kesho Agosti 10 na 11, ambapo atapokelewa hiyo kesho wilayani
Sengerema akitokea Chato mkoani Geita alikokuwa na mapumziko mafupi.
“Rais Magufuli atawasili kesho
asubuhi katika mkoa wetu akitokea Chato mkoani Geita na ataanza ziara
katika wilaya ya sengerema kwa ajili ya kuwasalimia wananchi, kuwapa
taarifa za mikakati na maendeleo awamu ya tano pamoja na utekelezaji wa
ilani ya uchaguzi”. Amesema Mongella.
Pia amesema hiyo kesho Rais
Magufuli atasimama maeneo mbalimbali kwa ajili ya kuwasalimu wananchi
kabla ya kuwasili wilayani Nyamagana.
Ametanabaisha kwamba Rais
Magufuli ataitimisha ziara yake kesho kutwa agost 11, kwa kukagua ujenzi
wa daraja la watembea kwa miguu la Furahisha Jijini Mwanza, pamoja na
upanuzi wa barabara ya Furahisha hadi Pasiansi ambapo ataweka jiwe la
msingi katika ujenzi wa miundombinu hiyo.
Mongella amewasihi wananchi kujitokeza kwa wingi katika
mkutano wa hadhara utakaofanyika kuanzia majira ya saa nanne mchana
katika uwanja wa Furahisha ambapo Rais Magufuli atahutubia wananchi
baada ya kukagua miradi hiyo ya ujenzi.
Tags
HABARI KITAIFA