![]() |
| Ndugai akizungumza na wafanyakazi wa ofisi ya Bunge katika uwanja wa ndege wa Dodoma alipofika akitokea Jijini Dar es laam IMEANDALIWA NA BANDA BLOG |
![]() |
| Spika wa Bunge Job Ndugai akielekeza jambo wakati alipokuwa akiongea na waandishi wa habari hawapo pichani, katika chumba cha kupumzika cha uwanja wa ndege wa Dodoma jana, Kushoto ni Mke wake Dkt. Fatma Mghana |
![]() |
| Spika akisaini kitabu cha wageni uwanjani hapo |
![]() |
| Akimshukuru Mke wake Dkt, Fatma Mgana kutokana na kujitoa kumhudumia wakati alipokuwa akitibiwa Nchini India |
Na John Banda,Dodoma
SPIKA wa Bunge la
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Job Ndugai amehamia rasmi Dodoma huku akiahidi
kulitafutia ufumbuzi suala la wabunge wa Ukawa kususia vikao vya bunge.
Kauli hiyo
aliitoa jana,Mjini hapa alipowasili katika uwanja wa Ndege wa Dodoma akitokea
Jijini Dar es Salaam ambapo awali alikuwa nchini India kwa Matibabu.
Alisema jambo
linalomuumiza kichwa ni wabunge kutosalimiana pamoja na kutoshirikiana katika
mambo mbalimbali hivyo kuahidi
kulishughulikia kwa kukaa pamoja na pande zote.
“Tatizo langu mimi ningependa tuelewane na
wabunge, ilifikia wakati mahusiano ya wabunge wa pande hizi mbili yalikuwa
mabaya mno , kama mnakumbuka sehemu kubwa ya kipindi kile cha mwezi wa Ramadhani ilifika mahali hata mtu
fulani akitengeneza futari watu wa upande fulani hawawezi kwenda kula futari wabunge ni timu moja lazima
tushirikiane’’alisema
Uendeshaji
wa Bunge na wabunge kukosea kanuni
Alisema katika
mabunge mengine kila bunge jipya la zamani linapomalizia muda wake linapitia
kanuni mpya na bunge linalokuja watu wapya linakuta kanuni zilizorekebishwa na
walioondoka
“Sisi mwaka 2007
tulirekebisha tuliokuwa bungeni sio jambo zuri kwani unatengeneza sheria wakati
wewe ni mchezaji, sheria zinatakiwa kutengenezwa na watu wengine halafu
wachezaji wanaenda kucheza kwa kutumia sheria zilizotengenezwa” alisema
Alisema kwa
utaratibu uliopo kanuni zipo, spika na wenzake wanatakiwa kutilia mkazo na
wabunge wazielewe na kuzitekeleza wameshatoa semina na makongamano ya kutosha
na wako tayari kuelimisha wabunge kama kuna haja ya kufanya hivyo.
“Kama kuna kanuni
ambazo wabunge wanaona zina matatizo makubwa, tunao muda wa kupendekeza hivyo
kwa spika na tunayo kamati maalum tunaita kamati ya kanuni ambayo ikipokea
mapendekezo ya namna hiyo inafanyiwa kazi yakishafanyiwa kazi huwa lazima
mapendekezo hayo yaende kwenye bunge zima ili wabunge wote wakubali hiki
kibadilike hiki hakikuwepo kiingizwe au hiki kitoke” alisema
KUHAMIA DODOMA
Kuhusina na
kuhamia Dodoma,Ndugai alisema ofisi yake imeishahamia rasmi huku wale waliokuwa
wakifanya kazi Dar es salaam nao watajiunga katika siku za hivi karibuni.
‘’Wote tumekuja
Dodoma tulikuwa na ofisi ndogo Dar wote watakuja Dodoma watabaki wachache tu
kwa ajili ya suala la afya pamoja na wale wanaotaka kusafiri’’alisema
mwisho
Tags
Bunge





