BANDA MEDIA BLOG

TPB YAPEWA MAAGIZO 4 YA KUFANYIA KAZI LIKIWEMO LA KUWAKOPESHA WATU WA HALI ZA CHINI ILI KUWEZA KUBORESHA ZAIDI UTENDAJI WAKE

Mbubunge wa jimbo la Same Mashariki akizungumza kwenye kikao hicho
Mkurugenzi Mkuu Mtendaji wa Benki ya Posta Tanzania Sabasaba Moshingi akifanua jambo wakati akiwaongoza watendaji wa Bemki hiyo kuhojiwa na kamati ya kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali [PAC], vikao hivyo vimeanza rasmi mjini humo kutokana na hatua ya serikali kuhamishia shuhuli zake makao makuu ya nchi.

Msajili wa Hazina Laulence Mafulu akizungumza jambo kwenye kikao hicho IMETENGENEZWA NA BANDA BLOG

Mwenyekiti wa Bodi ya Benki ya Posta Tanzania Professa Lettice Rutashobya akitoa ufafanuzi wa jambo kwenye kikao hicho
Wajumbe wa kamti ya PAC na watendaji wa TPB wakiwa kwenye kikao hicho

Mkurugenzi wa Sheria na Katibu wa Benki ya Posta Tanzania Mystica Mapunda Ngongi akizungumza jambo wakati alipotakiwa kufafanua moja ya swali la wabunge wa kamati ya PAC mjini Dodoma waliokaa ni wataaramu wa Benki hiyo
kikao kikiendelea
Watendaji wa TPB wakiwa ukumbini hapo

Na John Banda, Dodoma
MSAJILI wa Hazina,Lawrence Mafuru amekiri kuwa bado kuna msururu wa mashirika ya umma ambayo kila siku yanapanga foleni Hazina kwaajili ya kusaidiwa huku mengine yakisaidiwa kulipiwa mishahara ingawa ya yanafanya biashara.

Kauli hiyo aliitoa jana katika kikao cha Kamati ya bunge ya hesabu za serikali(PAC) ilipokuwa ikihoji hoja za Mkaguzi Mkuu wa hesabu za serikali(CAG) kwa benki ya posta Tanzania, mjini hapa.
Mafuru alisema kwasasa  inajidhihirisha na kuondoa hisia kuwa mashirika ya umma yanayomilikiwa na serikali hayawezi kuendeshwa kwa ufanisi.
Alibainisha licha ya hisia hizo lakini bado Hazina kuna msururu wa mashirika yanayosaidiwa ingawa yanajiendesha kibiashara.
“Lakini hapa tunapata ushahidi tukiyasimamia vizuri mashirika yetu na kuyasaidia yanaweza kujiendesha na kuleta tija na kupata faida,”alisema Mafuru
Hata hivyo alisema kwa jitihada zilizofanywa na benki ya posta inapeleka meseji kwa mashirika mengine kwamba hakuna kisingizio inawezekana kujiendesha kwa ufanisi na tija.
Alisema maagizo  yaliyotolewa na kamati hiyo yatasaidia benki ya posta kufikia malengo yake.
“Benki iendelee kujiimarisha na kuyafanya mashirika mengine yatakayoingia kwenye kamati ya PAC kujipanga na kuonesha kwa namna gani inaweza kuwasaidia watanzania kwa kujiendesha kwa faida kupitia miradi ya maendeleo, naipongeza Benki hii kwa sasa kujiimarisha tofauti na ilipokuwa mwanzo,”alisema Msajili huyo
Alibainisha benki hiyo kwasasa ipo kibiashara na ipo kwenye nafasi ya juu kati ya zaidi ya benki 50 na kwamba taasisi kama hizo kwasasa zinatakiwa kujiendesha kibiashara na kuyataka mashirika mengine kujifunza katika hilo.
Mafuru alisema inawezekana kujiendesha na kutengeneza faida badala ya kuwa tegemezi na hivyo utamaduni huo uigwe na mashirika mengine.

Nae mkurugenzi mkuu mtendaji wa Benki hiyo Sabasaba Mwashingi aliainisha ukuaji wa mtaji wa Benki hiyo kwa kipindi cha miaka 5 kutoka billion 8.mwaka 2010 mpaka billion 41 mwaka 2015 ambapo ukuaji huo unatokana na faida zinazotengenezwa na wenyewe
Alisema kuhusu mikopo mtaji umekua kutoka Bilion 66 walizoanzia mwaka 2010 mpka kufikia billion 252 mwishini mwa mwaka 2015.
Kwa upande wake, Mwenyekiti wa kamati hiyo, Aeshi Hilaly, aliipongeza benki hiyo kwa kufikia mtaji wa sh. Bilioni 41 ambapo alisema ilikuwa kwenye mtaji wa chini sana hapo awali na kuonekana ikielekea kusuasua lakini sasa ni tofauti na miaka ya nyuma.

Naye Mwenyekiti wa bodi ya benki hiyo, Profesa Lettice Rutashobya, alisema atashughulikia mapungufu yaliyojitokeza katika ukaguzi ili mwaka ujao kusiwe na hoja hizo.
Aidha alisema atahakikisha benki hiyo inajiimarisha na hatarudi katika hali iliyokuwa awali kutokana na mikakati iliyopo ikiwa ni pamoja na kufunga mifumo mbalimbali ili kuwa na uwezo wa kushindana na benki zingine. 
Mwisho.

Post a Comment

Previous Post Next Post
BANDA MEDIA BLOG
BANDA MEDIA BLOG
BANDA MEDIA BLOG