Katibu Mktendaji wa Bodi ya Filamu Tanzania (KBF) Bibi. Joyce Fissoo.
…………………………………………………………………..
Na: Frank Shija, MAELEZO
SERIKALI imepongeza juhudi za
wadau wa Tasnia ya Filamu nchini kutokana na jitihada zao katika
kuhakikisha tasnia hiyo inakuwa na kuwaletea maendeleo endelevu ikiwemo
Ajira za uhakika kwa vijana.
Pongezi hizo zimetolewa na Katibu
Mktendaji wa Bodi ya Filamu Tanzania (KBF) Bibi. Joyce Fissoo
alipokutana na ujumbe kutoka Taasisi isiyo ya Kiserikali ya TYEOO
walipomtembelea ofisini kwake jana kwa ajili ya kutambulisha rasmiMradi
wa TYEEO Barazani entertainment jana Jini Dar es Salaam.
Fissoo alisema kuwa mradi huo ni
muhimu kwa mustakabari wa kukuza tasni ya Filamu nchini kwani utarahisha
kufikisha katika kuwafikia wadau wengi zaidi wa tasni hiyo walioko
katika mikoa ya pembezoni.
“Niseme tu kwa dhati kabisa
nawapongeza sana kwa ubunifu wenu mradi huu ni mzuri na utaongeza tija
katika tsni yetu ya Filamu, name nina waahidi kuwapa ushirikiano pindi
mtakapo kuwa mnahitaji”. Alisema Fissoo.
Aidha alitoa ushauri kwa Taasisi
hiyo kutumia vibanda vya maonyesho ya Filamu vilivyopo katika maeneo
mbalimbali nchini ili kutekeleza mradi huo kwa kuwa nia ya Serikali ni
kuona dhana ya urathimishaji wa kazi za wasinii inafanikiwa.
Kwa upande wake Mkurugenzi
Mtendaji wa TYEEO, John Kallaghe amesema kuwa pamoja na kuwa mradi huo
ni binafsi lakini kutokana na imani kubwa waliyonayo juu ya Bodi ya
Filamu wameona siyo busara kuendelea kutekeleza jambo kubwa kama hili
bila ya kushirikisha mamlaka hiyo ambayo ndiyo msimamizi mkuu wa Tasnia
ya Filamu nchini.
Aliongeza kuwa wazo la kuanzishwa
kwa mradi huu ilikuwa ni kusaidia kuwawezesha vijana kujikomboa katika
lindi la umaskini kupitia huduma itokanayo na mradi huu ambayo ni
utayarishaji na usambazaji wa kazi za wasanii wa Filamu kwa njia ya
kisasa zaidi.
Kallaghe alisema kuwa wao kama
wadau tasni hiyo wako tayari kupokea ushauri na maelekezo ya namna
ambavyo wanaweza kuboresha na kutekeleza mradi huo kwa ajili ya
maendeleo ya taifa kwa ujumla.
Mradi wa TYEEO Barazani ni
miongoni mwa miradi kadhaa ambayo imeanzishwa na taasisi ya TYEEO,
ulioasisiwa tangu mwaka 2013 na unakadiriwa kutoa fursa ya ajira za
uhakika kwa vijana takribani 6000 katika kada zote za Filamu hadi
kufikia mwaka 2017.
Tags
KIBURUDANI