Taarifa iliyotolewa leo September
15 2016 na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi, imeeleza kuwa Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli, amemteua
Mhandisi Emmanuel Korosso kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Kampuni ya Ndege
Tanzania (ATCL).
Taarifa hiyo imesema kuwa uteuzi wa
Mhandisi Emmanuel Korosso unaanza mara moja. Mhandisi Emmanuel Korosso
anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Salim Msoma ambaye alimaliza muda
wake.
Wakati huo huo, Rais
Magufuli amemteua Mhandisi Ladislaus Ernest Matindi kuwa Mkurugenzi Mkuu
wa Kampuni ya Ndege Tanzania (ATCL). Kabla ya uteuzi huu Mhandisi
Ladislaus Ernest Matindi alikuwa Mkurugenzi katika Shirika
linaloshughulikia masuala ya usafiri wa anga Barani Afrika (EGNOS-Africa
Joint Programme Office) lenye makao yake nchini Senegal.
ULIKOSA HII YA RAIS MAGUFULI KUSEMA WANALALAMIKA PESA ZIMEPOTEA…HII MSG IENDE CLEAR KWAO? UNAWEZA KUANGALIA VIDEO HII HAPA CHINI
Tags
HABARI KITAIFA