Jumuiya ya Umoja wa
vijana wa CCM imemsimamisha kazi aliyekuwa Katibu wa.UVCCM Mkoa wa
Arusha Ezekiel Mollel kwa kutotiii agizo la Makao Makuu linalomtaka
kuhama na kusababisha mvutamo na malumbano yasio na tija kwa chama cha
Mapinduzi mkoani Arusha.
Pia Jumuiya imewataka
vijana wa uvccm kutambua kuwa shughuli za uendeshaji wa umoja huo
zinafanyika kwa kufuata taratibu za kikanuni chini ya misingi ya nidhamu
na utii.
Kaimu katibu mkuu wa
uvccm shaka Hamdu Shaka amewaeleza wandishi wa habari katika ofisi za
UVCCM mkoa wa Arusha mara baada ya kumaliza mzozo ulioibuka na
kusababisha baadhi ya vijana kufunga ofisi wakimkataa Ezekiel asiendelee
kubakia mkoani hapo.
Shaka alisema tokea
tarehe 25 August makao makuu ilimuandikia barua Mollel kumuhamishia
Makao Makuu Dar Es Salam lakini cha ajabu kwa muda wote amekuwa
akikaidi kuhama kwa sababu zake binafsi.
Alisema kikao cha
sekreterieti ya Taifa kilichoketi jijijini Dar es salaam 14 September
kimeamaua kumsimamisha kazi katibu huyo na kumtaka ampishe katibu wa
mkoa mpya Said Goha aliyehamia Arusha akitokea lindi
“Mollel amekuwa akidai
kuwa Arusha kuna harufu ya ubadhirifu wa mali na miradi ya Jumuiya,
Makao makuu haijapinga dai hilo , kuhama kwake si kikwazo cha kuzuia
kubaini nani amehusika na tuhuma hizo, amehishwa kwa sababu za kawaida
pia kutokana na sintofahamu iliopo “alisema shaka.
Alipoulizwa iwapo ni
mpango wa kukuondoa ili kuficha ukweli wa ufujaji wa miradi alisema
kuhama kwake hakuwezi kuzuia ukweli usijukikane, kwani Jumuiya inafanya
uchunguzi wa miradi na rasilimali zake pia vyombo vya serikali vimeombwa
viingiliie sakata hilo ili kupata ukweli wa mambo.
“Mtumishi unapohamishwa
toka kituo kimoja kwenda kingine na kukataa huo ni uvunjaji wa
taratibu, ukiukaji wa kanuni na kutoonyesha nidhamu ya kazi,
amesimamishwa kazi hadi jambo lake litakapifikishwa katika vikao vya
kitaifa vyenye mamlaka ya uteuzi wake wa mwisho kwa mujibu wa kanuni ya
UVCCM”alieleza shaka
Akijibu swali la
mwandishi kwamba katibu huyo amekuwa akikaidi kuondoka kwa sababu
analindwa na baadhi ya wakubwa wa makao Makuu pia makao makuu ikitaka
kumlinda kiongozi mmoja wa juu asihusishwe na ubadhirifu huo, shaka
alikana na kusema wanaoeneza maneno hayo ni mashabiki wa kisiasa..
“Nasema vijana wenzetu
wa Arusha wafahamu uendeshaji wa kazi zetu ni uzingatiaji wa taratibu na
kikaanuni, makao makuu haiwezi kumkingia kifua mwizi na kumtetea ,
kumlinda na kumtetea mvunja taratibu husika “alisema.
Aidha Kaimu huyo Katibu
mkuu alisema kazi ya ufuatiliaji miradi, mikataba , mapato na matumizi
yake yatafuatiliwa hatua kwa hatua na ukweli wa jambo hilo utaanikwaa
bila mtu kulindwa na kuogopwa.
Hata hivyo shaka
alipoulizwa kwamba makao makuu imeshindwa kumchukulia hatua za
kinidhamu mwenyeikiti wa mkoa huo Lengi Sabaya anayedaiawa kufanya hadaa
na kukutwa na vitambulisho feki , alijibu kuwa madai hayo ni binafsi
yenye mwekeleo wa jinai na iwapo kweli anakabiliwa na tuhuma hizo
vyombo vya dola vipo na vinapaswa kuchukua hatua haraka UVCCM
haitamlinda mtu katika jambo lolote lililo kinyume na maadili ya Chama.
Pia akiwataka wana
Jumuiya kuacha tabia ya kubuni au kubashiri mambo ambayo mtu hana
ushahidi nayo akidai kwamba kiongozi fulani anamlinda mtu fulani wakati
hakuna kiongozi makini anayeweza kumlinda mtu anayekiuka kanuni na
kuvunja taratibu halali
“chama chetu kina Katiba
jumuiya yetu ina kanuni toleo la 2012 tuna kanuni ya utumishi kanuni ya
fedha na maadili iyo ndio miongozo yetu katika kutekeleza majukumu ya
kila siku hatutafumbia macho mtu yoyote atakaepindisha mstari mmoja wa
kanuni au taratibu kwa vile hakuna aliye juu ya miongozo hiyo” alisema
shaka
Amewataka vijana wa
Arusha kuwa watulivu kwani viongozi wote wako makini katika kila jambo
na jumuiya Arusha itaendelea kubaki salama.
Shaka amewasili mkoani
arusha jana kufuatia kuibuka kwa mzozo uliosabanisha baadhi ya vijana
kumfungia ofisi katibu aliyehamishwa Ezekiel molel ambae anaungwa mkono
na Mwenyekiti wa UVCCM wa mkoa huo kwa madai amempa kazi afanye na
hajakamilisha.
Tags
SIASA