Habari kubwa zinazotrend sasa hivi mtu wangu moja nii hii iliyoripotiwa
na kituo kikubwa cha habari Kenya cha Citizen kupotea kwa Rais wa
Malawi, Peter Mutharika ambae hajarudi nchini
kwake tangu alivyoondoka
kuelekea New York Marekani kwenye mkutani mkubwa wa Umoja wa Mataifa kwa
mujibu wa rekodi imetajwa kuwa aliondoka nchini New york, September 15
2016 na mpaka sasahivi hajawasili nchini kwake Malawi.
Rais Mutharika amepotea kwa muda wa wiki 3 tangu sasa aondoke nchini
kwake na imepelekea raia wa nchi hiyo kuweka hashtags kwenye mitandao ya
kijamii zikisema #bringbackMutharika haswa kwenye twitter kama
unavyoona hapo chini.