Kwenye vitu ambavyo inawezekana hukua ukifahamu au kufikiria
kama kuna uwezekano wa kuwepo ni pamoja na hii issue ya upatikanaji wa
mafuta aina ya
Diesel kwenye visima vya maji Mkoani
Songwe.

Waziri wa Mazingira na Muungano Ofisi ya Makamu wa Rais Mhe
January Makamba kwenye ziara yake ya mazingira amefanikiwa kufika katika
mji wa Mloo
ulioko kwenye mkoa wa Songwe na kupokea taarifa ya mazingira ya Mkoa
ambayo imebainisha tatizo la uwepo wa mafuta ya Diesel kwenye visima vya
maji na kuelezwa kuwa mafuta hayo siyo mafuta ghafi yanayotakiwa
kupatikana ardhini.

Taarifa
hiyo pia imeeleza kuwa uvamizi wa shughuli za binadamu katika vyanzo
vya maji inatishia uhai wa vyanzo hivyo,Waziri Makamba ameahidi kusaidia
upatikanaji wa wataalamu ili kuweza kutambua chanzo cha tatizo hilo la
uwepo wa mafuta katika visima vya maji na kutambua njia sahihi za
kukabiliana na tatizo hilo.

Vilevile
Waziri Makamba amefika katika
Wilaya ya Ileje
ambapo pia amepokea taarifa ya Mazingira ya Wilaya na kupongeza juhudi
kubwa za wilaya ya Ileje katika utunzaji wa mazingira hasa eneo kubwa
la misitu uliopo katika lililopo katika Wilaya hiyona kuahidi pia
kuzisaidia Halmashauri za Wilaya na Vijiji namna sahihi na bora zaidi ya
kuandaa sheria ndogo za mazingira ili kukabiliana na changamoto za
uharibifu wa Mazingira.
Umemiss kuyafahamu Mambo 7 ya kutikisa treni ya kisasa,Utata Mamilioni ya Lipumba na mengine?Bonyeza play hapo chini kutazama.