Mchungaji
Bruno Mwakibolwa kutoka Kanisa la EAGT Mito ya Baraka Temeke Jijini
Dar es salaam, jumapili iliyopita Oktoba 16, 2016 alihudumu katika
Kanisa la EAGT Lumala Mpya la Sabasaba Ilemela Jijini Mwanza, baada ya
kuwasili katika kanisa hilo akitokea nchini Kenya.
Ilikuwa
Ibada iliyojaa neema ambapo Mchungaji Mwakibolwa aliwahimiza waumini wa
Kanisa la EAGT Lumala Mpya kumtumia Mungu kwa moyo wa kweli na
watabarikiwa maishani mwao.
Alisema
ziko njia mbalimbali za kumtumikia Mungu ikiwemo kuhakikisha waumini
wanajikita katika kumjengea Mungu Makanisa bora ili kuwezesha neno la
Mungu kusonga mbele.
Na BMG
Viongozi mbalimbali wakiwa kwenye ibada katika Kanisa la EAGT Lumala Mpya Jijini Mwanza
Kiongozi wa timu ya kusifu na kuabudu, EAGT Lumala Mpya akihudumu katika ibada hiyo
Waumini wa EAGT Lumala Mpya Jijini Mwanza wakiwa kwenye ibada hiyo
Waumini wa EAGT Lumala Mpya Jijini Mwanza wakiwa kwenye ibada hiyo
Hii pia ni miongoni mwa njia bora kumtumikia Mungu
Kutoka
kushoto ni Mchungaji wa Kanisa la EAGT Mito ya Baraka Jijini Dar es
salaam, Bruno Mwakibolwa, Mchungaji wa Kanisa la EAGT Lumala Mpya Jijini
Mwanza, Dkt.Daniel Moses Kulola pamoja na Mama Mchungaji, Mercy Daniel
Kulola.
Mmoja wa waumini wa EAGT Lumala Mpya Jijini Mwanza akiwa kwenye ibada hiyo
Waumini wa EAGT Lumala Mpya Jijini Mwanza wakiwa kwenye ibada hiyo.
Tags
HABARI ZA DINI









