BANDA MEDIA BLOG

Mtazamo wa ‘King Kibadeni’ kuelekea mabadiliko ya Simba na Yanga


Abdallah Kibaden 'King Kibaden (kushoto) na Mrage Kabange wakati wakifatilia kwa karibu mchezo kati ya JKT Ruvu dhidi ya Mtibwa Sugar
Mchezaji wa zamani wa Simba na timu ya taifa ya Tanzania ambaye kwa sasa ni mwalimu wa soka Abdallah Kibadeni ‘King Kibadeni’ ameunga mkono mabadiliko ya mfumo wa uendeshaji kwa klabu kongwe nchini za Simba na Yanga akisema mchezo wa soka kwa sasa ni biashara.
Kibaden amesema mabadiliko hayo ya mfumo yafanyike kwa njia sahihi lakini si kwa njia za mkato kama zinazotaka kutumika hivi sasa.

“Katika maendeleo yoyote, kitu cha kwanza ni pesa ziwepo ili mambo yanayotakiwa kufanyika yaweze kufanyika. Pia lazima wawepo wataalam husika wa hilo jambo ambalo linatakiwa kufanyika,” amesema Kibadeni wakati akitoa maoni yake kuhusu mfumo wa mabadiliko ya kiuendeshaji unaotaka kufanywa na vilabu vya Simba na Yanga.
“Tukizungumzia kwenye soka, huko nyuma kwenye miaka ya nyuma watu walianzisha hivi vilabu kwa ajili ya kukutana mahali kuzungumza ni mahali ambapo walikuwa wanakutania, hakukuwa na biashara ya soka.”
“Sasahivi soka ni pesa kwasababu wachezaji wanalipwa, kuna vitu vingi vinahitajika ili kuiweka timu sawa ukianzia wachezaji, majengo, viwanja sasa vyote hivyo bila pesa haiwezekani. Kama tutasimama vilevile kama tulikotoka kwamba tucheze mpira kwasababu ya utani wa Simba na Yanga haiwezekani.”
“Inatakiwa tupate wataalam wa kutuelimisha na wataalam wa kutusaidia kutuonesha mipango halisi ya kufanya kuweza kwenda kwenye biashara ya mpira ambayo inataka umakini. Kama tutapata watu wa kutuelimisha na kutufundisha jinsi gani ya kuingia kwenye hiyo mifumo si vibaya, lakini kwa ujanja-ujanja italeta matatizo ndiyo maana wengine wanakubali wengine wanakataa lakini pesa zinahitajika.”
“Kuwepo kwa matajiri wanaotaka kuwekeza kwenye vilabu si tatizo hata huko nyuma tulikuwa na wafadhili lakini wafadhili wa nyuma walikuwa sio wale ambao wanataka nao wapate kitu ndani yake, walikuwa wanaweza kutusaidia kutuweka kambini na kununua jezi.”
“Hii biashara inayokuja sasahivi inawezekana ndiyo itakayoleta maendeleo inatakiwa watu waifahamu hiyo biashara inaendaje, sio wakae watu wawili au watatu hapana. Lazima kuwe na watu ambao wanafahamu haya mabadiliko yataendeshwaje na watu watafaidika vipi.”

Post a Comment

Previous Post Next Post
BANDA MEDIA BLOG
BANDA MEDIA BLOG
BANDA MEDIA BLOG