Na John Banda, Dodoma
Shirika lisilo la kiserikali la ICS linalojishuhulisha na miradi ya maji vijijini na kwenye mji midogo inayokua, limeanzisha mfumo wa malipo ya kabla ya kupatiwa huduma ya maji ambao utaziwezesha mamlaka za maji kujiendesha, tofauti na ule wa sasa wa kulipia baada ya kutumia ambao umewafanya watu, taasisi na mashirika binafsi na ya kiserikali kukatiwa huduma hiyo kutokana na kulimbikiza madeni.
Akiongea mjini Dodoma Meneja Mauzo wa Taasisi isiyo ya kiserikali ya ICS yenye makao makuu yake Nchini Uholanzi Abraham Mwanyamaki amesema miradi mingi ya maji imekuwa ikifa kutokana na kushindwa kujiendesha kunakosababishwa na madeni ambapo amesema mfumo huo wa malipo ya kabla utawezesha kupatikana fedha zitakazosaidia uendeshaji huo.