Baada ya uchaguzi wa Rais wa Marekani kumalizika na mshindi kutangazwa kuwa ni Donald Trump wa chama cha Republican, imeripotiwa kuwa Maelfu ya watu wameandamana katika miji mbalimbali nchini Marekani kupinga ushindi wa Donald Trump
Imeelezwa kuwa wengi wamekusanyika nje ya jumba maarufu la rais huyo mteule Trump Tower mjini New York wakipaza sauti zao dhidi ya msimamo wa Trump kuhusu sera za uhamiaji, mapenzi ya jinsia moja na haki ya uzazi yanayopingwa na Donald Trump. Wanasema hata dunia ina wasiwasi juu ya ushindi wake.
Source; Reuters, BBC
Tags
SIASA