BANDA MEDIA BLOG

ZAMALEK YAIFUMUA ARAB CONTRACTORS LIGI KUU YA MISRI.

zamalek-vs-contractors-e1457884434844
Na.Alex Mathias.
Timu ya Zamalek imeendelea kuchanja mbuga katika Ligi Kuu ya Misri baada ya kuwabugiza Arab Contractors jumla ya magoli 3-0 mchezo uliochezwa kwenye uwanja wa Taifa wa Cairo uliopo katika mji mkuu wa Misri, Cairo.

Kiungo mkabaji mwenye rasta raia wa Nigeria,Stanley Ohawuchialikuwa wa kwanza kuipatia goli timu yake katika dakika ya 20 baada ya kuachia shuti kali lililojaa wavuni licha ya kutanguliwa wageni waliendelea kuwabana vilivyo wenyeji hadi mapumziko Zamalek walikuwa mbele.
Kipindi cha pili kilianza kwa timu zote kufanya mabadiliko hata hivyo waliopata faida walikuwa wenyeji kunako dakika ya 76,Ismail Salahalifunga goli la pili akitumia ujanja wa kuwatoka mabeki na dakika ya 77 mkongwe Shikabala alifunga la tatu na kuihakikishia timu yake kuondoka na pointi zote tatu.
Kwa matokeo hayo Zamalek wamefikisha pointi 17 wakiwa wamecheza mechi saba na wapo katika nafasi ya sita huku wakiwa na viporo vinne kutokana na kuwa walipewa mapumziko baada ya kutoka kwenye michano ya klabu bingwa Afrika kwa kufika Fainali na kufungwa na Mamelodi Sundowns jumla ya magoli 3-1.
Kinara wa Ligi hiyo ni timu ya Misri El-Maqasah wenye pointi 27 wakiwa wamecheza mechi 10 wakati wapinzani wakubwa wa jadi wa Zamalek wapo katika nafasi ya pili wakiwa na pointi 26 Al-Ahly ambao Leo watakuwa ugenini kucheza na Nasra Tadeen huku nao wameshacheza mechi 10.

Post a Comment

Previous Post Next Post
BANDA MEDIA BLOG
BANDA MEDIA BLOG
BANDA MEDIA BLOG