Mwendesha pikipiki maarufu kwa
jina la bodaboda akiwa amejipumzisha katika eneo lililoathiriwa na
uharibifu wa mazingira unaofanywa na binadamu katika kijiji cha
Ormapinu, Arusha Desemba 17, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Ngombe na mbuzi wakiwa
wamesongamana chini ya mti pekee uliokuwepo katika eneo lililopo
karibu na Shule ya sekondari ya Oljoro mkoani Arusha wakifuata kivuli
ili kujikinga na jua Desemba 17, 2016. Uharibifu wa mazingira
unaosabishwa na shughuli za binadamu hasa ukataji miti hovyo unaathiri
hata viumbe wengine kama picha inavyoonyesha. (Picha na Ofisi ya Waziri
Mkuu)
Wananchi wakiwa wamebeba bango
lenye maneno yanayoeleza suala la uharibifu wa mazingira kuwa ni tatizo
kwao katika mkutano uliohutubiwa na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa kwenye
kijiji cha Ondenderet, Arusha Desemba 17, 2016. (Picha na Ofisi ya
Waziri Mkuu)
Tags
MAZINGIRA