Uongozi
wa Coastal Union kutoka mkoani Tanga inayoshiriki Ligi Daraja la Kwanza
Tanzania Bara, unawataka wapenzi wake waliopo Dar es Salaam kesho
(Jumapili Januari 1, 2017) kufika uwanja wa Karume zilipo ofisi za
Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), ili kushuhudia timu mpya na yenye
uwezo wa hali ya juu.
Kwa
mujibu wa Meneja wa timu Hilal Said, vijana wa sasa ni wapya nah ii ni
mechi ya pili tangu mzunguko wa pili uanze. Hivyo usajili mpya
umeonyesha mwanga na vijana wanapiga soka la uhakika.
“Naweza
kusema sisi hatustahili kucheza na timu za ligi daraja la kwanza, hata
ligi kuu hakuna timu ya kutufunga kwa sasa tumekua level nyingine
kabisa. Inafika wakati hata tukifanya mechi za majaribio tunaona kama
tunazionea timu tunazocheza nazo.
“Hivyo
nawaomba wapenzi wa soka si lazima wawe wa Coastal Union tu bali mpenzi
yeyote anayependa kuona soka la uhakika aje Karume kesho Jumapili.
Tunafungua mwaka kwa kuichapa Kimondo mabao yasiyo na idadi,” alisema
Hilal.
Coastal
Union inayoshika nafasi ya tano katika kundi B kwa sasa ina point sita
huku Kimondo FC kutoka beya ikishika mkia kwenye kundi hili.
Mchezo
uliopita Coastal Union ilitoka sare ya 1-1 dhidi ya Polisi Morogoro
katika uwanja wa Jamhuri mkoani Morogoro huku mashabiki wa soka mkoani
humo wakisifia kiwango kikubwa kilichoonyeshwa na wachezaji wa Coastal
Union.
Katibu
wa Coastal Union, Tahbit Abuu, aliweka wazi kuwa kwa sasa timu yoyote
itakayoingia katika anga zao watarajie kichapo kwani wanataka
kuhakikisha mechozote sita zilizobaki wanashinda ili kujiweka katika
nafasi nzuri.
“Tunataka
turudi ligi kuu, hakuna namna nyingine zaidi ya kuendeleza kichapo
popote pale iwe nyumbani au ugenini, kwa sababu timu ya ushindani tunayo
na uwezo tunao, hatuna sababu ya kuwa wanyonge,” alisema.
Wachezaji
wa Coastal Union wameshawasili jijini Dar es Salaam tangu Ijumaa ambapo
wamefichwa katika kambi maalumu kwenye moja ya fukwe za Bahari ya Hindi
tayari kwa mechi ya Jumapili.
Mwisho
Habari hii imetolewa na msemaji wa Klabu Hafidh Kido
Tags
MICHEZO KITAIFA