![]() |
| Mchungaji Kiongozi wa Kanisa la Winners Chapel Charles Prosperity akisisitiza jambo mbele ya waumini wa kanisa hilo wakati alipokuwa akihubiri kwenye ibada ya kumshukuru Mungu kwa ajili ya Chrismas |

![]() |
| Waumini wa kanisa hilo wakilisakata Rhumba walipokuwa wakimsifu Mungu wakati wa Ibada ya Chrismas iliyofanyika katika kanisa la Winners Chapel lilipo Ilazo mjini Dodoma [PICHA NA JOHN BANDA] |
![]() |
| Mahubiri yakiendelea |




![]() |
| Mchungaji akiwa katika picha ya pamoja na Kwaya ya Kanisa |
![]() |
| Mchungaji na mama Mchungaji akiwa katika picha ya pamoja na Wahudumu wa kanisa hilo |
Na John Banda, Dodoma
WATANZANIA wameshauriwa kutumia fedha kwa nidhamu hasa katika kipindi hiki cha sikuu za mwisho wa Mwaka ili kuepuka kuwa ombaomba au ufundi wa kukwepa madeni katika mezi ya mwanzoni mwa mwaka ujao wa 2017 ambao utakaribishwa saa 6 usiku wa Desemba 31. Mwaka huu
Ushauri huo ulitolewa jana kwenye ibada ya Chrismas na Mchungaji wa kanisa la Winners Int’ I Chapel Charles Prosperity ambapo alisema imejengeka tabia ya watu kutumia kila kitu bila kuweka akiba wakati wa sikuu huku baadae kushindwa kumudu maisha
Mchungaji huyo alisema kila mtu aweke akiba kwa ajili ya kesho kwa kuwa si busara kutumia kila kitu kilichotunzwa kwa muda mrefu na wakati mwingine mwaka mzima kwa siku moja tu na kisha siku moja au mbili hujikuta hata chakula hamna.
Prosperity alisema imekuwa kawaida hata kwa wakristo inapofika mwezi wa kwanza wakati wa kulipa ada au kodi ya pango wanabaki wanahaha kwa kukosa fedha ambayo wakati mwingine kunachangiwa na matumizi makubwa yanayofanywa wakati wa sikuku
“wapo watanzania wengi wakiwemo wakristo inapofika sikukuu ya Chrismas na ile ya mwaka mpya hujikuta wametumia mpaka kiasi cha mwisho kutokana na kupika aina mbalimbali za vyakula kukaribisha marafiki, kununua nguo hata kama hakubajetia, kula au kunywa kwenye mabaa au mahotel tofauti na nyumbani na mwishowe humaliza kila kitu na kesho hubaki akipiga miayo asijue cha kufanya
La muhim kuliko yote ni hili chagueni vitu vya kula isiwe umekaribishwa mahali basi ukala kila kitu kinachowekwa mezani wakati vipo vingine ambavyo hujawahi kuvitia tumboni ambapo kesho yake unabaki unaugua tumbo kutokana na mchafuko nawaambia kuweni waangalifu na muweke akiba ya fedha na vyakula ili kuepuka kulia kesho”, alisema
Aidha aliongeza kuwa Watanzania walio wengi wameigeuza siku ya Chrismas kuwa siku ya kugombana na wakati mwingine hata mahusiano ya kindoa kuvunjika kutokana na siku hiyo kudhaniwa kuwa ni siku ya kula, kunywa, kuvaa na kufanya mambo ya kujionyesha kwa wengine bali siku hiyo ni ya Wokovu wa Mungu aliyemtoa Yesu kwa ajili ya watu wake
Wengine wamegombana na kushindwa kuelewana kisa mwenzi wake kukosa fedha za kiatu,nguo au vitu vingine vya anasa
Chrismas siyo siku ya kuvaa, kunywa,kula
Tags
HABARI ZA DINI








