Muda mfupi uliopita kocha Phiri ameidokeza mbeyacityfc.com
kuwa amekamilisha maandalizi kwa kufanya marekebisho makubwa kwenye
mapungufu kadhaa yaliyoonekana kwenye michezo miwili iliyopita
yaliyoiacha City ikiambulia pointi mbili za suluhu mbele ya Kagera Sugar
na Toto Africans ya Mwanza.
Mchezo wa kesho ni muhimu, tumejitahidi kurekebisha mapungufu yote yaliyokuwepo kikosini kwenye michezo miwili iliyopita,vijana wangu wako ‘fiti’ na wameniahidi watafanya vizuri, ni jambo jema kusikia hivyo kutoka kwao hii ni kwa sababu kila mmoja anataka tushinde, wapo wachezaji kadhaa tutawakosa kwa sababu ni wagonjwa, Danny Joram na Omary Ramadhani hawakuwepo kabisa kikosini.
Kuhusu kiungo Mrisho Ngassa na
mshambuliaji Zahor Pazzi, kocha Phiri amesema wanaweza kuwa sehemu ya
kikosi cha kesho lakini watalazimika kuanzia kwenye bechi na kuingia
baadae hii ni kwa sababu wamefanya mazoezi kwa siku chache hivyo hawako
sawa asilimia 100.
Hawako fiti asilimia
100, watakuwepo kikosi lakini tunaweza kuwatumia kipindi cha pili, siku
mbili nyuma Ngassa alikuwa anasumbuliwa na tumbo, leo amefanya
mazoezi mapesi, kwa mujibu wa daktari ni wazi hatuwezi kumtumia muda
wote wa mchezo, hivyo hivyo kwa Pazzy ambaye amefanya mazoezi kwa siku
tatu sasa.
Tags
MICHEZO KITAIFA