BANDA MEDIA BLOG

SAMATTA APIGA GOLI LA MWAKA,KRC GENK IKILAZIMISHWA SARE LIGI KUU YA UBELGIJI


mbwana-samatta-genk_qhfzkxffpj151j64aurq7ix16
Na.Alex Mathias.
Klabu ya Genk ya Mshambuliaji wa Tanzania MBwana Ally Samatta imeshindwa kutamba katika uwanja wake wa nyumbani wa Cristal Arena mjini Genk baada ya kulazimishwa sare ya kufungana magoli 2-2 na timu ya Stardard Liege mchezo wa Ligi Kuu ya Ubelgiji.

Genk walikuwa wa kwanza kupata goli kupitia kwa Omar Colley dakika ya 3 baada ya kuwapiga chenga mabeki wa Stardard hata hivyo goli hilo halikuweza kudumu kwani mnamo dakika ya 15 Orlando Sa aliweza kuwasawazishia wageni.
Alikuwa Ishaka Belfodil alipigilia msumari wa pili dakika ya 25 na kuwanyamazisha wenyeji Genk hadi timu zinaenda mapumziko Stardard Liege walikuwa mbele wa kwa magoli 2-1.
Kipindi cha pili kilianza kwa timu zote kufanya mabadiliko huku Genk wakiweza kukokasa nafasi nyingi za kufunga na katika dakika ya 59 Stardard Lieg walipata pigo baada ya mchezaji Isaac Mbenza kuoneshwa kadi nyekundu na kubaki pungufu uwanjani.
MBwana Ally Samatta alionesha thamani yake ya pesa waliyomsajilia kutoka TP Mazembe akifunga goli la kusawazisha kwa Genk dakika ya 77 kwa kichwa akiunganisha krosi ya Thomas Buffel na likiwa goli lake la nne kwenye Ligi hiyo.
Kwa Matokeo hayo Genk ya Samatta imeshuka hadi nafasi ya 10 ikiwa na pointi 24 wakati timu ya Stardard Liege wakibaki kwenye nafasi yao ya nane wakiwa na pointi 28.
VIKOSI:KRC GENK:Marco Bizot,Omar Colley,Sandy Walsh|Jere Uronen,Sebastien Dewaest,Wilfred Ndind,Timothy Castagne,Alejandro Pozuelo,Nikos Karelis,Leandro Trossard|Thomas Buffel,Leon Bailey,Mbwana Samatta.
STARDARD:Guillaume Hubert,Reginal Goreux,Elderson,Milos Kosanovic,Edmilson Junior|Corentin Fiore,Andrien Trebel,Konstantinos Laifis,Ibrahima Cisse,Benito Raman|Isaac Mbenza,Orlando Sa|Jean-Luc Dompe,Ishaka Belfodil.

Post a Comment

Previous Post Next Post
BANDA MEDIA BLOG
BANDA MEDIA BLOG
BANDA MEDIA BLOG