BANDA MEDIA BLOG

TAIFA JANG’OMBE YAANZA VYEMA MAPINDUZI CUP,YAICHAPA TAIFA BOYS


jang
Michuano ya Mapinduzi Cup inayofanyika visiwani Zanzibar imefunguliwa jana usiku kwa mahasimu wa jadi Taifa Jang’ombe na Taifa Boys mchezo uliopigwa kwenye uwanja wa Aman,Zanzibar huku Taifa Jang’ombe wakiibuka na ushindi wa bao 1-0.

Mshambuliaji Seif Hassan ‘Banda’amekuwa mchezaji wa kwanza kufungua acounti ya magoli katika michuano hiyo baada ya kuifungia Taifa Jang’ombe dakika za jioni 84 Mpira ulikuwa wa kona ndipo ikiwa piga ni kupige na kumkuta mfungaji akiwa kwenye nafasi nzuri.
Mechi hiyo ilikuwa na upinzani mkubwa kutokana na timu zote kutoka mtaa mmoja hivyo kukamiana na kutambiana nje na ndani ya uwanja kulisababisha mechi hiyo kuwa ya upinzani mkali.
Kwa matokeo hayo Taifa Jang’ombe inaongoza kundi A ikiwa na alama tatu mkononi huku ikiwa na timu za URA toka Uganda ambao ni mabingwa watetezi pamoja na wekundu wa msimbazi Simba ya jijini Dar es salaam.
Baada ya mchezo huo, Kesho (Jumamosi) hakutakuwa na mechi, Jumapili ratiba ya Mapinduzi itaendelea lakini mechi inayosubiriwa kwa hamu ni kati ya Taifa Jangombe dhidi ya Simba SC ambayo inatarajiwa kuwasili Zanzibar kesho (Jumapili).

Post a Comment

Previous Post Next Post
BANDA MEDIA BLOG
BANDA MEDIA BLOG
BANDA MEDIA BLOG