Wabunge 29 wa Bunge la Korea kusini wamejiondoa katika chama tawala nchini humo.
Hatua
hiyo imekuja kufuatia tuhuma za rushwa ambazo pia zinamgusa Rais wa
nchi hiyo Park Geun-hye kwa mashtaka ya kutumia madaraka vibaya.Hatua hiyo imekuja ikiwa imebaki miezi michache kufanyika kwa uchaguzi wa Rais.
Wabunge hao wanatarajiwa kuunda chama kingine kipya na upo uwezekano wa kumtaka Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa anayemaliza muda wake Ban Ki-Moon, kuwa mgombea wa chama hicho.
Tags
Bunge