Kamanda wa Polisi wa Jeshini (MP) katika ikulu ya Gambia, Luteni Nuha
William Jammeh, yasemekana yupo mafichoni. Inasemekana alitoroka Gambia
siku chache zilizopita. Kamanda huyu alitoa amri ya kukamatwa kwa
maafisa kadhaa wa jeshi la nchi hiyo walioonekana kumpinga Rais
aliyemaliza muda wake, Yahya Jammeh.
Kwa sasa Luteni Nuha Jammeh hajulikani alipo. Amekimbia mji mkuu wa
Banjul na inaaminika kuwa amekimbilia nchini Senegal. Namba yake rasmi
ya simu inayojulikana inaonesha kuwa yupo nchini Senegal ingawa simu
yake imezimwa.
Akimzungumzia Nuha Jammeh, mtu aliyewahi kusoma nae darasa moja alisema:
” Alikuwa mkimya sana na anayependa sana dini. Ilikuwa ni rahisi sana
kuzoeana naye kipindi kile. Baada ya kukutana na Yahya Jammeh, huwezi
jua, kwa maana yule dikteta alikuwa na uwezo wa kugeuza watu wazuri
kabisa kuwa mashetani.”
Tags
KIMATAIFA
