BANDA MEDIA BLOG

JULIO AAMUA KUCHOMA VYETI VYAKE MOTO



kiw
Kocha Jamhuri Kiwelu Julio,amesema kwamba kwa sasa hana mpango wa kurejea katika kazi yake ya ufundishaji wa mpira wa miguu hapa nchni kwa kuwa mpira wa Tanzania umetawaliwa na siasa ambazo hazina msingi.

jamhuri-kihwelo-mwadui-fc_m0d7t4cbpjks1gsdb7za19b84
Julio ameiambia fullshangweblog.com kwamba licha ya kutakiwa na timu mbalimbali za hapa nyumbani,lakini kwake hafikirii kabisa swala hilo kwani anaamini Tanzania hakuna watu wanaofahamu vizuri uendashaji wa mpira wa miguu.
Amesema kwamba viongozi wengi ni wababaishaji na wamejawa na majungu ambayo hayana msingi katika uendelezaji wa mchezo huo unaopendwa Zaidi ulimwenguni.
Aidha amedai kuwa anaamini ipo siku ataita waandishi wa Habari ili washuhudie jinsi atakavyochoma moto vyeti vyake ili umma utambue kuwa dhamira yake ya kutofundisha soka iko palepale wala sio jambo la mzaha.

Post a Comment

Previous Post Next Post
BANDA MEDIA BLOG
BANDA MEDIA BLOG
BANDA MEDIA BLOG