Kocha wa Manchester City Pep Guardiola anakaribia kustaafu kufundisha soka na hataitakuwa miaka 65 kama alivyodhani awali.
Muispania huyo amewahi kuifundisha klabu ya Barcelona kwa mafanikio makubwa kisha Bayern Munich kabla ya kuchukua nafasi ya Manuel Pellegrini Man city.
”Nitakuwa hapa Manchester kwa
misimu ama mitatu labda na zaidi,” Guardiola mwenye miaka 45 alisema
kabla ya ushindi wa magoli 2-1 dhidi ya Burnley.
”Sitakaa kwenye benchi mpaka miaka 60-65.Nafikiri mchakato wa kuanza kusema kwaheri umekaribia.
Guardiola ameshinda vikombe 14
katika miaka minne akiwa na Barcelona, ikiwa ni pamoja na vikombe vitatu
vya La Liga na viwili vya ligi ya mabingwa Ulaya.
Alipumzika mwaka mzima kabla ya
kujiunga na Bayern Munich na kuwaongoza kupata vikombe vitatu vya ligi
kuu licha ya kukosa ligi ya mabingwa Ulaya
Kikosi cha Guardiola kilicheza
pungufu baada ya Fernandinho kupewa kadi nyekundu lakini magoli ya Gael
Clichy na Sergio Aguero yaliwapa ushindi.
Tags
MICHEZO KIMATAIFA