Habari kutoka Jijini Mbeya, zimeeleza sema kuwa Mwenyekiti wa CCM wilaya
ya Mbeya Mjini, Ndugu Ephrahim Mwaitenda mwenye umri wa miaka (60)
amenusurika kifo baada ya kupigwa risasi mgongoni na mtu au watu
wasiofahamika.
Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya, Emmanuel Lukula amesema tukio
hilo limetokea mnamo tarehe 29. 01. 2017 majira ya saa 05. 45 usiku
katika kitongoji cha Ilopa, Kijiji cha Mahenge, Kata ya Makwele, Tarafa
ya Ntebela, wilayani Kyela Mkoa wa Mbeya.
Amesema tukio hilo limetokea wakati akiwa amelala Kitandani nyumbani
kwake Ntebela, ambapo mbinu iliyotumika ilikuwa ni kukata wavu wa
dirisha na kumjeruhi kwa kutumia silaha za kienyeji zinazotumia risasi
za goroli.
Taarifa zaidi zimeeleza kuwa, Mwenyekiti huyo amefikishwa Hospitali ya Rufaa Mbeya na hali yake inaendelea vizuri.
Kamanda Lukula, amewaambia waandishi wa habari kuwa nia ya shambulizi
hilo ilikuwa ni kutaka kumuua na kwamba juhudi za kuwatafuta na
kuwakamata wahusika zinaendelea Kulia ni Kaimu Katibu wa CCM Mkoa wa
Mbeya ndugu Lobe Zongo akimpokea Mwaitenda katika hospitali ya rufaa
Mbeya wakati alipofikishwa hospitalini hapo CCM wilaya ya Mbeya mjini
ndugu Ephrahim Mwaitenda akifikishwa hospitalini hapo
Tags
HATARI
