Wachezaji wa Arsenal Olivier Giroud, Laurent Koscielny na Francis Coquelin wameongeza kandarasi zao na klabu hiyo.
Arsenal haijatangaza kuhusu
kiwango cha kandarasi hizo ,lakini Koscielny amesema katika mtandao wa
Twitter kwamba ataongeza kandarasi yake hadi mwaka 2020.
”Tunafurahi kwamba wachezaji
watatu muhimu wameamua kusalia nasi kwa kipindi cha muda mrefu”,
Mkufunzi wa Arsenal Arsene Wenger amenukuliwa akisema.
Wachezaji hao wa Ufaransa wamekuwa
wakishiriki kila mechi huku Giroud akiweka kandarasi hiyo baada ya
kufunga mabao manne katika mechi nne likiwemo bao lake la ‘nge’ dhidi ya
Crystal palace.
”Francis ameimarika pakubwa katika kipindi cha miaka michache iliopita kwa sababu ana maono kila siku”, alisema Wenger.
”Olivier ana uzoefu katika mechi
kubwa na ameimarika zaidi tangu ujio wake hapa. Koscielny ni kiungo
muhimu wa kikosi chetu na ninaamini ni mmojawapo wa mabeki wazuri
duniani”.
Tags
MICHEZO KIMATAIFA