Wizara ya Nishati na Madini
inapenda kuufahamisha umma kuwa, Awamu ya Kwanza ya Watumishi wa Wizara
kuhamia Makao- Makuu ya Nchi, Dodoma inaanza tarehe 10 Februari, 2017.
Miongoni mwa watakao hamia
katika awamu hiyo ni pamoja na Viongozi na Watendaji Wakuu wa Wizara
ambao ni Waziri wa Nishati na Madini, Naibu Waziri wa Nishati na Madini,
Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini na Naibu Makatibu Wakuu wa
Nishati na Madini.
Watumishi wengine ni pamoja na
Kamishna wa Madini Tanzania, Kamishna wa Nishati na Masuala ya Petroli,
Mkurugenzi Msaidizi wa Utawala na Maafisa. Jumla ya Watumishi
wanaohamia Dodoma Awamu ya Kwanza ni 47.
Aidha, kutokana na uhamisho huo, anuani ya Wizara Dodoma ni;
Katibu Mkuu,
Wizara ya Nishati na Madini,
Barabara ya Kikuyu,
S.L.P 422,
DODOMA
Imetolewa na;
KATIBU MKUU
WIZARA YA NISHATI NA
Tags
HABARI KITAIFA