Wakati Arsenal imekuwa ikisifiwa kwa
soka safi na la pasi nyingi lakini katika mechi ya Ligi ya Mabingwa
dhidi ya Bayern Munich, mambo yalikuwa tofauti kabisa.
Arsenal imepoteza mechi hiyo kwa mabao
5-1 na kama hiyo haitoshi hata pasi ilizopiga ni za chini sana
ukilinganisha na Bayern Munich waliokuwa nyumbani.
Wenyeji Bayern walipiga pasi 704
zilizofika huku Arsenal wakipiga 186 pekee zilzofika ikiwa ni chini
karibu ya mara tano jambo ambalo linaonyesha kweli walizidiwa kila
idara.
Tags
MICHEZO KIMATAIFA

