MUIGIZAJI wa sinema za Kibongo, Abdul Ahmed ‘Ben’ amedaiwa kupima
maambukizi ya virusi vya ugonjwa hatari wa Ukimwi (Ngoma) na kukimbia
akidaiwa kuhofi a majibu.
Chanzo makini kililitonya gazeti hili kuwa muigizaji huyo alionekana
kwenye kituo f’lani cha afya maeneo ya Kigogo jijini Dar akipima Ukimwi
lakini alipokuwa akisubiri majibu kwenye benchi, ghafl a alitimka na
kuondoka eneo hilo.
Alipopigiwa simu na mwanahabari wetu na kuelezwa mchongo mzima, Ben
alishtuka na kukiri lakini akadai si kwamba alikimbia bali alipata
dharura na atarejea kuyachukua majibu. “Nimepata dharura, pale nitarudi
tu kuchukua majibu si kwamba nimekimbia moja kwa moja,” alisema Ben.
Tags
AFYA
