NAHODHA wa Yanga, Nadir Haroub ‘Cannavaro’, amerusha kombora Simba baada
ya kusema watahakikisha wanaifunga timu hiyo katika mchezo wa Ligi Kuu
Tanzania Bara, ili waweze kuwa katika mazingira bora ya kutetea ubingwa
wao.
Akizungumza jana, Cannavaro alisema mchezo huo utakaochezwa Februari 25 mwaka huu, utaamua hatima ya wao kutetea taji lao.
Cannavaro alisema wamejipanga kuondoka na pointi tatu ambazo zitawaweka
katika mazingira bora zaidi ya kuongoza katika msimamo wa ligi hiyo na
baadaye kutetea ubingwa wao.
“Simba acha wachonge, lakini dawa yao ni sana,” alisema Cannavaro.
Alisema wanapiga kelele huku wakijua wazi hawana uwezo wa kuifunga Yanga.
“Sisi tunawaheshimu Simba kama zilivyo timu nyingine katika ligi, lakini
pia hatuwaogopi kwa kuwa tunajua dawa yao iko wapi hawawezi kupata
ubingwa kupitia sisi,” alisema.
Tags
MICHEZO KITAIFA
