Waziri wa Sheria na Katiba Dkt. Harrison Mwakyembe, amepongeza jitihada
za Rais Magufuli za kupambana na dawa za kulevya huku akisimulia
alivyoshindwa vita hiyo wakati alipokuwa Wazri wa Uchukuzi, hususan
katika Uwanja wa Ndege wa Dar es Salaam
Amesema alipata taarifa za kichunguzi kuhusu jinsi dawa za kulevya
zinavyopitishwa katika uwanja wa ndege wa Dar es Salaam, na akaamua
kutangaza vita akisaidiana na mtu ambaye hajamuweka wazi, lakini mwisho
mtu huyo aliyekuwa akiongoza vita hiyo, aliishia kufungwa gerezani mpaka
leo.
Mwakyembe amesema hata baada ya yeye kutumia nguvu zake kumtoa gerezani
ameshindwa, jambo ambalo linaonesha kuwa vita dhidi ya dawa za kulevya
ni ngumu kuliko kawaida, huku akionesha matumaini kuwa katika awamu hii,
serikali itashinda.
Dk. Mwakyembe amezungumza hayo jijini Dar es Salaam, alipokutana na
wahadhiri na wanafunzi kutoka Shule Kuu ya Sheria ya Chuo Kikuu cha Dar
es Salaam, kwa lengo la kupokea mapendekezo ya kanuni ya kusimamia
sheria mpya ya msaada wa kupata msaada wa kisheria iliyopitishwa na
Bunge hivi karibuni.
Tags
BIASHARA HARAMU
