Mara baada ya kupata taarifa za Watanzania wenzetu ' kufurumushwa '
nchini Msumbiji niliweza kufanya mazungumzo na Mtanzania mmoja aitwae
Bwana Hamidu ni Mfanyabiashara mkubwa kati ya Tanzania, Msumbiji na
Afrika ya Kusini na kwa Wale Watanzania muishio Afrika ya Kusini hasa
mji wa Cape Town kati ya Mtaa wa Mowbry na Randebosch mtakuwa mnamjua
sana huyu Hamidu na amewahi pia kuishi mno Kibiashara nchini Msumbiji.
Mazungumzo yangu na Kaka Hamidu yalilenga hasa katika kutaka kujua nini '
Kiini ' cha kilichowakuta Ndugu zetu Watanzania huko ugenini nchini
Msumbiji na ndipo akaniambia sababu kadhaa ambazo naziweka hapa Kwenu
ili mzijue na ikiwezekana tuzijadili.
Na ikumbukwe nimesukumwa pia kulifuatilia hili suala hasa kwa kuangali
Uhusiano mzuri katika tena wa Kindugu ambao uliwekwa vizuri kabisa na
Waasisi wa nchi zetu hizi mbili Hayati Mwalimu Nyerere na mwenzake
Hayati Samora Machael.
Bwana Hamidu alisema kuwa vinavyotugharimu Watanzania hasa tuwapo
ugenini na ndivyo pia vimewagharimu wenzetu waliokuwa nchini Msumbiji ni
vifuatavyo:
Uwizi uliotukuka na hasa wa Simu na Magari, Matusi na kuwadharau Wazawa.
Uuzaji uliotukuka kabisa wa Dawa za Kulevya na hasa hasa Bangi / Bange.
Kuendekeza ' ushirikina ' wetu tuliotoka nao Tanzania na kuwaroga Wenyeji bila huruma.
Kutopenda kufanya Kazi na kuishi kwa ' kuomba omba ' sana hadi wametuchoka.
Umalaya na hapa hakuficha akasema kuwa Wanaume wa Kitanzania wanapenda
sana ' kuwabandulia ' Wasumbiji wake zao na Wanawake wa Kitanzania ni '
maarufu ' kwa kupenda ' kubanduana ' na Wanaume wa Msumbiji.
Majungu. Hapa alisema kuwa Watanzania wakiwa wanatafuta Kazi au wawapo
Kazini huku hupenda mno kuwapiga ' Majungu ' wazawa kwa Matajiri ili
wafukuzwe Kazi kisha wabakizwe wao na ambapo na Wao pia huwaleta Ndugu
zao wengi kutoka nchini Tanzania.
Utapeli uliotukuka kwa wanaowafanyia Wazawa wananchi wa Msumbiji. Na
katika hili Bwana Hamidu alisema kuwa si jambo geni uwapo nchini
Msumbiji kumsikia Mtanzania uliyemjua tokea huku huku Bongo akiitwa
Kassim lakini huyo huyo ukikutana nae Maputo huko anaitwa George na
ukibahatika tena kukutana nae mji wa Cabo Delgado utasikia anaitwa
Benjamin na wamekuwa wakiwatapeli Wasumbiji huku wakihama hama miji ili
kujificha na wasijulikane na waweze kufanikisha wanachokitaka na maisha
yanaendelea.
Wandugu hizo ndizo sababu ambazo Mmoja wa Watanzania ambaye ameishi sana
huko Bwana Hamidu amenipa na kasema kuwa hakuna Watu ' Wavumilivu '
kama Wasumbiji ila kwa vitendo hivyo saba ( 7 ) nilivyoviorodhesha hapo
uvumilivu wao Kwetu Watanzania umewashinda na kama ' mbwai mbwai ' tu.
Naomba kuwasilisha na nimshukuru tu Bwana Hamidu wa Cape Town Afrika ya
Kusini kwa ushirikiano wake mkubwa juu ya kunifunulia nini hasa kiini
cha tatizo la Watanzania wenzetu ' kufurumushwa ' nchini Msumbiji.
Tags
KIMATAIFA
