Baada ya kashikashi za hapa na pale ya wasanii wa bongo movie kuingia
kwenye siasa huku Wema Sepetu akihamia CHADEMA na kusema anaidai CCM,
swahiba wake, Batuli amekanusha. Wakati vita vya maneno vikiendelea,
mwenzao, Irene Uwoya amewachana.
Irene ametumia ukurasa wake wa Instagram kuandika maneno yenye busara ndani:
Katika maisha siku zote ushauri unaruhusiwa kutolewa au kupokelewa…
Lakin sio lazima mtu kupokea ushauri unaotolewa… Kila mtu anauhuru
wakuamua kitu ambacho anahisi kinamfaa kwenye maisha sababu… Sazingine
kwenye maisha Kuna sehemu inafika unacho jiskia kwenye moyo wako sio
rahisi mtu mwingine kujiskia … Sasa ni mbaya sana kuishi kwa hisia…
Ifikie Wakati tujitaidi kuheshimu hisia Za mtu… Lakin pia kunavitu
vingine nazani Nivyema vkabaki kwa wausika wavinaowahusu…yani sio lazima
kuongea kila kitu kwenye jamiii… Watu wanatamani sazingine kuskia vtu
ambavyo wanahisi vinafaida kwa Jamaniii… Kunavitu vingine ukiongea
havina maana.”
Tags
KIBURUDANI
