Bunge limepitisha kwa kauli moja, azimio la kuitwa Mkuu wa Mkoa wa Dar
es Salaam, Paul Makonda na Mkuu wa Wilaya ya Arumeru, Alexander Mnyeti
ili kuhojiwa na Kamati ya Haki, Kinga na Madaraka ya Bunge.
Azimio hilo lililopitishwa leo lilitokana na hoja iliyowasilishwa na
Mbunge wa Ukonga, Mwita Waitara akisema wateule hao wa Rais wametoa
kauli zinazodhalilisha hadhi ya mhimili huo wa Dola.
Akijibu swali kuhusu tuhuma dhidi yake zilizoibuliwa na wabunge kuhusu
chanzo cha mali zake, Makonda aliwaambia waandishi wa habari kuwa wakati
mwingine watunga sheria hao hulala bungeni kwa kukosa cha kuzungumza.
Kutokana na wabunge kukerwa na kauli ya Makonda, mbunge wa Mkuranga (CCM), Abdallah Ulega aliomba mwongozo kuhusu suala hilo.
Mkuu wa wilaya, Mnyeti anadaiwa kuandika kwenye ukurasa wake wa Facebook
kuwa wabunge ni wapuuzi kutokana na michango yao wakati walipohoji
hatua ya Ma-DC na Ma-RC kutoa amri za kuwaweka mahabusu viongozi wa
kisiasa.
Tags
Bunge
