Mhubiri mmoja nchini Afrika Kusini amekuwa akiwapa waumia sumu ya kuua panya kama moja ya njia ya kujaribu imani yao.
Light Monyeki, ambaye anaongoza kanisa la Grace Living Hope Ministries
mjini Pretorria, anasema kuwa kwa kunywa sumu hiyo, inaonyesha kuwa kifo
hakina nguvu kwa waumini.
Picha kwenye ukurasa wake wa Facebook, zinamuonyesha akichanganya dawa
inayotumiwa kuua panya wa chupa na kuinywa na kisha kuwapa waumini.
Bwana Monyeki ni mhubiri wa hivi majuzi kuripotiwa kuhusika na visa vyenye utata kanisani.
Tags
HABARI ZA DINI
