Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ameagiza Shirika la Ndege Tanzania (ATCL),
kujiridhisha na kiwango cha mapato linayokusanya kwa usafirishaji mizigo
iwapo kiko sahihi.
Majaliwa amesema hayo alipotembelea makao makuu ya ATCL jijini Dar es
Salaam kujionea utendaji tangu lilipoboreshwa mwaka jana kwa kununuliwa
na Serikali ndege mpya mbili.
Waziri Mkuu amemtaka Kaimu Mkurugenzi wa Fedha na Utawala wa ATCL, Witness Mbaga kuhakikisha anatekeleza suala hilo.
Pia, ametakaka viongozi wa shirika hilo kuhakikisha wanazingatia ratiba za njia na muda wa safari ili wasipoteze wateja.
Vievile amesema ataagiza uchunguzi ufanywe na Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu
wa Hesabu za Serikali (CAG) utakaolenga kujua ukusanyaji mapato katika
kipindi hicho.
Waziri Mkuu akasema Serikali haitakuwa tayari kushuhudia shirika hilo
linakufa tena na kuwataka viongozi wahakikishe linaendeshwa kwa faida
kwa manufaa ya Taifa.
Tags
USAFIRISHAJI
