BANDA MEDIA BLOG

MREMBO Agness Gerald (Masogange) Afikishwa Mahakamani Kisutu Aachiwa Kwa Dhamana


Video queen Agnes Gerald ‘Masogange’ amepandishwa kizimbani Jumatano hii katika mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu na kusomewa mashitaka mawili ya kutumia dawa za kulevya.


Mrembo huyo ambaye ni maarufu kwa kupamba video za muziki wa wasanii wa bongo fleva, amekana tuhuma hizo na kesi yake kuahirishwa hadi Machi 21 mwaka huu.

Katika mashtaka yake mawili yaliyosomwa na mwendesha mashtaka Mashauri Wilboard chini ya wakili wa serikali Constatine Kokulwa, Agnes anadaiwa kutumia dawa za kulevya aina ya Heroin na Oxazepan. kwa nyakati tofauti.

Mara baada ya kusomewa mashtaka yake, ameachiwa kwa dhamana ya wadhamini wawili pamoja na kusaini bondi ya shilingi milioni 10.

Pia mrembo huyo ambaye amewahi kukamatwa nchini Afrika Kusini akihusishwa na usafirishaji wa dawa za kulevya, ametakiwa kutotoka nje ya Dar es Salaam kwa kipindi chote cha kesi bila kibali cha mahakama

Post a Comment

Previous Post Next Post
BANDA MEDIA BLOG
BANDA MEDIA BLOG
BANDA MEDIA BLOG