Wakati ambapo wewe hujawahi kufika katika kila mkoa hapa Tanzania, kuna
mwanamke wa Marekani ambaye amefika kwenye kila nchi duniani.
Kama haitoshi, ameweza kufika katika nchi zote 196 ndani ya miezi 18 na
siku 26. Cassie De Pecol amevunja rekodi ya Guinness World iliyokuwepo
mwanzo.
Mwanamke huyo alianza safari yake July 2015, akipigia debe utalii
endelevu kama balozi wa taasisi ya International Institute of Peace
Through Tourism.
Jumla, De Pecol ametumia bajeti ya $198,000 kuizunguka dunia.
Tags
UTALII
