Taarifa ya Shirikisho la Mpira wa
Miguu Afrika (CAF), imethibitisha hilo pasi shaka kwamba Tanzania ndiyo
yenye nafasi ya kucheza fainali hizo zitakazofanyika kuanzia Aprili 2,
mwaka huu huko Gabon baada ya Madagascar kuenguliwa kutokana na
kutoandaa vema fainali hizo.
Taarifa hizo za CAF kutoka
Libreville, nchini Gabon zinathibitisha kwamba Kamati ya Utendaji ya CAF
imeipa ushindi Tanzania dhidi ya timu ya Jamhuri ya Congo ambayo katika
michuano ya kufuzu, ilimchezesha mchezaji Langa Lesse Bercy aliyezidi
umri kinyume cha kanuni za kanuni za michuano hiyo.
Serengeti Boys iliyosimamiwa na
Kamati ya Utendaji ya TFF chini ya Rais Jamal Malinzi, sera kubwa
ilikuwa ni kuangalia kuendeleza mpira wa miguu kwa vijana, ilikusanywa
na kuandaliwa kwa michezo mingi ya kimataifa ambako kwa mwaka moja tu
2016, ilicheza mechi zisizopungua 16 ya kimataifa.
Katika michezo hiyo ya kirafiki
na ushindani, Serengeti Boys ilipoteza mchezo wa 16 tu dhidi ya Congo
ilihali kulikuwa na rufaa kuhusu mmoja wa wachezaji wa Congo ambaye
alionekana kuwa na umri mkubwa. Mchezaji huyo ni Langa Lesse Bercy.
CAF, kwa nyakati tofauti ikiwamo
Novemba 10, 2016 na Desemba 15, mwaka jana walitoa agizo kwa Congo
Brazzaville kumpeleka kijana huyo Cairo, Misri kwa ajili ya vipimo vya
MRI ili kuthibitisha au kupangua madai ya Tanzania. Congo Brazzaville
hawakupeleka.
Januari 12, mwaka huu 2017
iliamriwa kwa mara nyingine kijana huyo kupelekwa jijini Libreville,
Gabon ili kufanyiwa vipimo vya MRI, lakini hakupelekwa na katika kikao
cha Kamati ya Utendaji ya CAF, kimeamua kumaliza suala hilo na kuipa
ushindi Tanzania.
Siku 10 ziliisha Januari 23,
mwaka huu lakini tangu hapo kumekuwa na maswali ya kutosha kuhoji nafasi
ya Tanzania yakitoka kwa Watanzania kupitia wanahabari, lakini TFF
ilisimama kidete kutangaza kuwa tunasubiri uthibitisho wa CAF ambayo leo
Februari 3, mwaka huu imetangaza rasmi kuwa Tanzania itacheza fainali
hizo.
Tags
MICHEZO KIMATAIFA