Mshambuliaji Kevin Sabato wa klabu ya Majimaji FC baada ya timu yake
kufungwa bao 3-0 dhidi ya Simba amefynguka na kusema kuwa Simba
wamebahatisha katika mchezo huo kuwafunga goli hizo tatu kwa sababu wao
waliwazidi Simba kimchezo.
Kevin Sabato amedai kuwa makosa waliyofanya uwanjani ndiyo yamepelekea
Simba kushinda mchezo huo na kuchukua ushindi pamoja na point tatu,
lakini kwa upande wake Mzamiru Yasini kiungo wa Simba amesema kuwa timu
yake ilikuwa vizuri kila kona ndiyo maana imeweza kuchukua pointi tatu
kwa kupata magoli matatu.
"Sisi tulijianda vizuri tukafanya vizuri kila sehemu ndiyo maana
tumeweza kuwafunga goli tatu Majimaji FC, unajua ligi ya mwaka huu ina
ushindani mkubwa sana hivyo ikitokea umepata nafasi unaitumia vizuri. Na
sisis tumepata nafasi ndiyo maana tumewapiga goli tatu hivyo naweza
kusema tuliwazidi sehemu zote" alisema Mzamiru Yasini
Tags
MICHEZO KITAIFA
