Mchezaji wa timu za Kisiju Pwani
kulia wa kushoto akijaribu kumtoa beki wa timu ya Lukanga Fc wakati wa
kivumbi cha mashindano ya ULEGA CUP hatua ya nusu fainai iliyopigwa
kwenye uwanja wa shule ya msingi mkuranga,Kisiju waliibuka na ushindi wa
bao 1-0 na kutinga hatua ya fainali.
Mchezaji wa timu ya Lukanga Fc wa
kushoto akiwa katika harakati zake za kuwapita wachezaji wa timu ya
Kisiju Pwani katika mchezo wa kwanza wa hatua ya nusu fainali ya
michuano ya ULEGA CUP kwenye uwanja wa shule ya msingi Mkuranga.
Wachezaji wa timu zote mbili wakiwa uwanjani kuisakata kabumbu katika mchezo wa nusu fainali hiyo.
(PICHA NA VICTOR MASANGU)
………………………………………..
NA VICTOR MASANGU, MKURANGA
TIMU mbili za soka za Kisiju Pwani
pamoja na Tengelea Fc zimefanikiwa kukata tiketi ya kutinga katika
hatua ya fainali baada ya kuibuka na na ushindi katika michezo miwili
waliyoicheza hatua ya nusu fainali kwenye kinyang’anyiro cha michuano
ya ‘ULEGA CUP 2016-2017 ’ kwenye uwanja wa shule ya msingi Mkuranga
mkoani Pwani.
Michuano hiyo ambayo imeandaliwa
na Mbunge wa Jimbo la Mkuranga Abdalah Ulega kwa lengo la kuweza kuibua
na kukuza vipaji vya wachezaji mchezo wa kambumbu ambao walishirikishwa
kutoka katika kata zote 25 zilizopo katika jimbo hilo.
Katiha mchezo wa hatua ya nusu
fainali ya kwanza iliweza kuzikutanisha timu ya Kisiju Pwani ambao
walimenyana na majirani zao wa karibu timu ya Lukanga Fc ambapo timu ya
Kisiju ndio iliyoweza kuchupa fainali baada ya kuibuka na ushindi wa
bao 1-0 dhidi ya wapinzani wao.
Bao la washindi katika mtanange
huo liliwekwa kimiani na mshambuliaji wao wa kutumainiwa Mudy Mbete
kunako katika dakika ya 71 baada ya kuachia shuti kali lilizozama moja
kwa moja langoni na kumwacha mlinda mlango wa timu ya Lukanga Fc
amebaki mdomo wazi.
Mchezo mwingi wa hatua ya nusu
fainali ya pili ambao ulikuwa unasubiriwa kwa hamu na shauku kubwa na
wadau na mashabiki wa mchezo huo timu ya ulizikutanisha timu ya
Tengelea Fc ambao walicheza na Mwandege ambapo Tengelea waliibuka na
ushindi wa bao 1-0 lililopachikwa na mchezaji Andrwe Joseph kunako
katika dakika ya 80 na kufanikiwa kupata nafasi ya kucheza hatua ya
fainali.
Kwa matokeo hayo timu ya Kisiju
Pwani pamoja na timu ya Tengelea Fc ambao ndio wameweza kushinda katika
michezo yao ya nusu fainali watakutana uso kwa uso katika mchezo wa
fainali unaotarajiwa kufanyika machi 5 mwaka huu kwenye dimba la shule
ya msingi Mkuranga.
Kwa upande wake Mbunge wa Jimbo la
Mkuranga Abdlah Ulega ambaye ndio mwandaaji wa mashindano hayo ya soka
alisema kwamba nia yake kubwa ni kuunda timu ya Jimbo ambayo itakuwa
ikishiruki katika ligi mbali mbali na ndoto yake kubwa ni kuhakikisha
nashirikina na wadau wa soka ili kuwa na kikosi kizuri amabcho kitaweza
kushiriki ligi kuu ya Tanzania bara katika siku za usoni.
Tags
MICHEZO KITAIFA