Korea Kaskazini kwa mara nyingine tena imefyatua kombora na kulielekeza
upande wa Pwani ya Japan. Maofisa wa kijeshi kutoka Korea Kusini
wamekadiria kombora hilo limesafiri umbali wa takribani kilomita 500
huku serikali ya Korea Kusini sasa imeitisha kikao cha kiusalama mjini
Seoul .
Maafisa wa Pentagon nchini Marekani nao wamesema wamelifuatilia tukio
hilo na kuongeza kuwa wamebaini ni kombora la masafa ya kadri.
Waziri wa mambo ya nje wa Korea Kusini amesema vitendo kama hivyo vya
uchokozi unaoendelezwa na Korea Kazkazini vinaonyesha dhahiri jinsi
utawala jirani yao huyo usivyo na makini huku wakipania kuwa na zana za
Nuclear.
Waziri mkuu wa Japan, Shinzo Abe ambaye angali ziarani Marekani,
ameshtumu ufyatuaji huo wa Kombora huku Rais Trump akimhakikishia Abe
kuwa anamuunga mkono asilimia 100.
Harakati hizo za ufyatuaji wa kombora zimekuja siku moja tu baada ya
mazungumzo kati ya rais wa Marekani Donald Trump na waziri mkuu wa Japan
Shinzo Abe mjini Washington, ambako wamekubaliana kulipa kipa umbele
swala la jinsi ya kukabiliana na vitisho vya zana za kinuklia kutoka
Korea Kazkazini..
Tags
KIMATAIFA
