Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda amemkabidhi Kamanda wa Polisi
Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Kamishna Simon Sirro majina mapya ya
watu wanaotuhumiwa kuhusika kwenye mtandao wa biashara ya Madawa ya
kulevya ambapo katika majina hayo wako askari 3, msanii wa muziki
Vanessa Mdee pamoja na video queen ambaye pia alikuwa mpenzi wa rapper
Young Dee, Tunda.
Aidha RC Makonda amesema wale walioitwa leo kituoni hapo bado
wanaendelea kufanya nao mahojiano na kama kuna yeyote atakayekutwa na
hatia sheria itachukua mkondo wake.
Akizungumza na waandishi wa habari Ijumaa hii, RC Makonda aliliagiza
jeshi la polisi kuwakama wale ambao hawajaripoti leo kama walivyoagizwa
jana huku akiwataka wale waliotajwa leo kuwasili Kituo Kikuu cha Polisi
Dar es salaam Jumatatu.
Tags
BIASHARA HARAMU
