BANDA MEDIA BLOG

WAZIRI LUKUVI AWATAKA VIONGOZI WA MIKOA YA TANGA NA MANYARA KUTEKELEZA AGIZO LA WAZIRI MKUU


LUKIO
Waziri wa Ardhi,Nyumba na
Maendeleo ya Makazi,William Lukuvi akizungumza  kwenye kikao cha pamoja
baina yake na viongozi wa mikoa ya Tanga na Manyara kuhusiana na mgogoro
wa mipaka uliopo kati ya wilaya za kilindi na kiteto ili kuona namna ya
kuumaliza
 Mkuu wa Mkoa wa Tanga,Martine Shigella akizungumza kwenye kikao
hicho.
 Mkuu wa Mkoa wa Manyara,DoktaJoel Bendera akizungumza kwenye mkutano huo kulia ni Kaimu Katibu Tawala wa Mkoa wa Tanga,Monica Kinala 

Baadhi ya wenyeviti wa
halmasahuri zote mbili na wakuu wa wilaya za Kiteto na Kilindi
wakifuatilia kikao hicho
Kushoto ni Mkuu wa wilaya ya Kilindi,Sauda
Mtondoo akifuatilia majadiliano hayo
WAZIRI wa ardhi Nyumba na
maendeleo ya makazi William  Lukuvi amewataka viongozi kutoka Mkoa wa
Manyara na Tanga kutekeleza agizo la Waziri Mkuu la kumaliza mgogoro wa
mpaka katika ya Wilaya ya Kilindi na Kiteto kwa kuhakiki upya mpaka huo
kupitia GN namba 65 ya mwaka 1961.
Lukuvi aliyazungumza hayo jana Mkoani hapa alipokutana na viongozi 
kutoka Mikoa ya Tanga na Manyara
kuhusiana na mgogoro uliodumu kwa miaka mingi kati ya Wilaya hizo mbili
ambapo aliwataka washirikiane kuhakikisha mgogoro huo unamalizika kama
Waziri Mkuu alivyoagiza pindi alipofanya zira yake  mkoani
hapa.
Aidha alisema kupitia Wizara ya ardhi imeteuwa wataalamu wa ardhi 
ambao hawatatoka kati ya Mikoa yenye
mvutano wa mgogoro huo ili kujenga imani kwa wananchi na watakuwa na
jukumu la kuhakiki upya mpaka huo kwa manufaa ya wananchi wa pande zote
mbili.
“Timu ya wataalamu kutoka wizara yangu imekwishaundwa kwa kufanya
kazi 
hiyo mategemo ya utekelezaji wa majukumu
hayo tunatarajia kuanza rasmi machi 1 mwaka huu na zoezi hili litadumu
kwa mwezi mmoja tu na wala hakuna ubabaishaji”Alisema Lukuvi.
Alisema hakuna mpaka mpya utakaokwenda kupimwa kati ya Wilaya hizo 
mbili zaidi ya kuhakiki ule wa awali
ambao unatokana na ramani ya mwaka 1961,zoezi hili la uhakiki lazima
wananchi na viongozi watambue kuwa linafanyika kwa  mara ya tatu na
litakuwa la mwisho.
Pia aliwataka viongozi wote kuanzia ngazi ya mkoa mpaka Kijiji

kushiriki vema katika zoezi hilo ili kuweza kujadiliana hasa pale
panapotokea mapungufu na waache kutatua mgogoro huo huku wakiwa na
matakwa yao binafsi na kufanya hivyo hakutamaliza mgogoro huo zaidi ya
kuuwongeza.
“Kama kuna viongozi wanamatakwa yao basi watambue hawatapata nafasi
na 
tayari tulishapokea agizo kutoka
Waziri Mkuu na kinachotakiwa hapa ni utekelezaji wa kumaliza mgogoro
huo”Alisema.
Kwa upande wake Mkuu wa mkoa Tanga Martin Shigela alisema jukumu
kubwa 
lililopo mbele yao ni kutoa ushirikiano
kwa timu iliyoundwa na Wizara hiyo na kuhakikisha wanafanikiwa kumaliza
mgogoro huo kwa wakati kama Waziri alivyoagiza.
Nae Mkuu wa Mkoa wa Manyara Joel Bendera alisema lazima viongozi 
washirikiane kwa pamoja kutatua mgogoro
huo ambao umekuwa ni tatizo kwa Wilaya hizo mbili na kupongeza hatua ya
Serikali ya uhakiki upya hasa kwa kufuata GN ya namba 65 ya mwaka 1961
kama alivyoagiza Waziri Mkuu na si vinginevyo.
Ikumbukwe siku kadhaa zilizopita Waziri Mkuu Kassim Majaliwa
alifanya 
ziara Wilayani Kilindi katika Kijiji cha
Mafisa na kuzungumza na wanachi Kijijini hapo kuhusiana na mgogoro huo
na kutoa maagizo kwa viongozi wa kuchaguliwa kuacha kutumia nafasi zao
vibaya kuongoza kwa mihemko au ushabiki kwa kuwa kufanya hivyo
kunapelekea wananchi kufuata ushabiki na kuvunja sheria zilizopo.
Majaliwa alisema katika ziara yake hiyo kuwa Aidha alisema baadhi
ya 
viongozi wa kisiasa na Serikali kwa
kutokuwa wa kweli mbele ya wananchi kuhusiana na mgogoro huo na
wanajaribu kufanya maamuzi kwa ajili ya maslahi yao ya kujiaminisha
mbele ya wananchi hao.
Alisema lazima ramani ya mwaka 1961 ifuatwe na viongozi waache kuwa
na 
agenda zao za siri na kuwadanganya
wananchi kwa kuanza kurudia kupima mpaka huo mara kwa mara bila ya
kupata majibu sahihi ramani na huu ni muda wa kuwael3za ukweli
wananchi
“Ramani ipo ya mwaka 1961 na najiuliza sana hivi hao wanaokuwa na 
tabia ya kurudia kupima pima mara
mbili agenda yao ni nini,huu si udanganyifu kwa wananchi?”Alihoji
Majaliwa.
Alisema kuananzia sasa GN itakayotumika ni ile namba 65 ya mwaka 
1961,zaidi wanachotakiwa wataalamu
kukifanya ni kuimarisha mpaka huo kwa kuwashirikisha  viongozi wa
Serikali,wanasiasa na wananchi ili kuweka mustakabali mzuri juu ya mpaka
huo
Habari kwa Hisani ya Blog ya
Kijamii ya Tanga Raha Blog

Post a Comment

Previous Post Next Post
BANDA MEDIA BLOG
BANDA MEDIA BLOG
BANDA MEDIA BLOG