Na.Alex Mathias
Mabingwa watetezi wa Ligi Kuu ya
Vodacom Tanzania bara Yanga wamelipa kisasi cha paka mwizi kwa wapiga
debe toka Shinyanga timu ya Stand United ambao wamekubali kichapo cha
magoli 4-0 Mchezo uliochezwa kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es
salaam
.
Donaldo Dombo Ngoma alifunga bao dakika ya 17 akipokea pasi ya Simon Msuva na kuukwamisha Mpira nyavuni kwa kichwa na dakika ya 26 Simon Msuva aliifungia Yanga bao la pili akimalizia pasi ya Ngoma.
Licha ya kufungwa magoli hayo mawili Stand United hawakukata tamaa kwani mnamo dakika ya 36 Selembe
alimanusura aifungie bao timu yake baada ya kuwachanganya mabeki wa
Yanga hadi Mapumziko wenyeji walikuwa mbele kwa magoli hayo mawili.
Kipindi cha pili kilipoanza tu Obrey Chirwa
aliwanyanyua tena mashabiki wa Yanga dakika ya 45 akifunga bao la tatu
baada ya kumpiga chenga Mlinda Mlango wa Stand United na dakika ya 58 Simon Msuva alikosa Penati baada ya kupiga shuti la juu.
Dakika ya 68 Nahodha Nadir Harub ‘Canavaro’
alipigilia Msumari wa nne baada ya kuunganisha Mpira wa Kona
iliyochongwa na Simon Msuva hadi dakika 90 zinamalizika Yanga wameibuka
na ushindi wa jumla ya magoli 4-0.
Kwa matokeo hayo Yanga wamefikisha
pointi 49 na kuendelea kukaa kileleni mwa Ligi Kuu ya Vodacom na nafasi
ya pili ikishikwa na Simba wenye pointi 45 ambao kesho nao watakuwa
ugenini mkoani Ruvuma kucheza na Majimaji
Tags
MICHEZO KITAIFA