Mabingwa
watetezi wa Kombe la FA Uingereza upande wa wawanawake Kina dada wa
Arsenal waliwalaza wapinzani wao Tottenham 10-0 na kufika robo fainali
Jumapili.
Danielle van de Donk alifungia
wenyeji hao mabao matatu, naye mshambuliaji wa zamani wa Sunderland Beth
Mead akafunga bao pia mechi yake ya kwanza kuchezea Arsenal.
Chelsea, ambao walishindwa na Arsenal fainali mwaka jana, pia walipata ushindi mkubwa, kwa kulaza Doncaster 7-0.
Bristol City walilaza Millwall 5-0.
Liverpool, Notts County, Birmingham na Sunderland pia walishinda kwenye mechi hizo za raundi ya tano.
Droo ya robofainali itafanyika baadaye Jumatatu.
Matokeo kamili mechi za raundi ya tano
- Manchester City 1-0 Reading (Jumamosi)
- Arsenal 10-0 Tottenham
- Birmingham 2-0 West Brom
- Bristol City 5-0 Millwall
- Chelsea 7-0 Doncaster
- Liverpool 2-1 (AET) Everton
- Notts County 3-2 Yeovil
- Sunderland 3-2 Aston Villa
Tags
MICHEZO KIMATAIFA