Fifa imetangaza kuifungia nchi ya Mali kushiriki michuano ya kimataifa kwa madai ya serikali kuingilia masuala ya soka.
Waziri wa Michezo wa
Mali, Housseini Amion Guindo aliamua kuunda kamati ya muda kuendesha
Shirikisho la Soka la Mali (Femafoot) baada ya kuona uongozi uliokuwa
madarakani kutokuwa sahihi.
Lakini baada ya
Femafoot kufikisha malalamiko yake Fifa, shirikisho hilo la soka la
limataifa, likaiamuru serikali ya Mali, kuvunja kamati hiyo hadi Ijumaa.
Baada ya kuona
hakukuwa na utekelezaji hadi leo usiku huku zikiwa zimebaki saw chache
kabla ya muda kufika, Fifa imetangaza kuifungia Mali.
![]() |
| BARUA YA FIFA KWENDA FEMAFOOT |
Katibu Mkuu wa Fifa,
Fatma Samoura alisisitiza serikali ya Mali kuachana na kuingilia michezo
na kutaka Rais wa Femafoot, Boubacar Baba Diarra aachwe aendelee
kuongoza.
Mwisho, Fatma Samoura
ndiye aliyeandika barua hiyo ya kuifungia Mali kushiriki michuano iliyo
chini yake, mambo ambalo bila shaka ni pogo kwa Mali.
Tags
FIFA
