Diamond Platnumz akihojiwa kwenye kipindi cha Clouds 360, ameulizwa
swali kuhusu wasanii kutangaza utalii wa Tanzania. Katika majibu yake
amesema kuwa serikali imeshindwa kuwekeza pesa kwa wasanii ili kutangaza
utalii na badala yake wanapoteza pesa nyingi kwa taasisi za nje.
Amesema kuwa kwa South Africa kupitia board yao ya utalii wana utaratibu
mzuri na wamewekeza kuhakikisha utalii wao unatangazwa na ndio maana
hata yeye ametumiwa kuutangaza utalii wa South Africa.
Amesema kwa hapa Tanzania alishawahi ku-apply TANAPA ili kuvitangaza
vivutio vya kitalii Tanzania lakini mwisho wa siku akapigwa danadana na
kuambiwa yeye inabidi ajitolee kuwa Goodwill Ambassador, sasa unakuwaje
goodwill ambassador wakati unatakiwa kuwekeza kwenye kutangaza vivutio!!
Unahitaji salio kwenye simu, nauli nk!!
Anasema serikali haioni thamani ya Mtanzania kabisa, wakati wasanii wana
wafuasi wengi wa ndani na kimataifa kwenye mitandao ya kijamii ambayo
wangeitumia kutangaza utalii.
Pia amesema suala la ku-shoot video Tanzania kuna vikwazo vingi sana
kama kupata maeneo na nyenzo nyingine. Hivyo wasanii kutumia gharama
kubwa kutangaza vivutio vya South Africa kwenye video zao.
Tags
Diamond Platnumz
